Friday, January 2, 2015

WALIOTEMBEA KUTOKA GEITA HADI DAR KUMWONA RAIS WAFIKIA MIKONONI MWA POLISI NA KUWEKWA SELO BADALA YA KUFIKIA IKULU

Vijana watatu wa CHADEMA waliotembea kwa miguu kutoka Geita hadi Dar es Salaam kumwona Rais wamewasili jijini Dar es Salaam leo.
Vijana hao walitaka kumwona Rais ili kuwasilisha ujumbe wao ikiwemo kutoridhishwa na kukithiri kwa vitendo vya kifisadi.
Hata hivyo vijana hao wamezuiwa kumwona Rais kutokana na kutokufuata taratibu za kumwona Rais ikiwa ni pamoja na kutokuomba vibali husika.
Akieleza maamuzi hayo Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alisema "Kuna utaratibu wa kumwona Rais uliotakiwa kufuatwa. Pia kama wametembea kutoka Geita bila vibali husika basi wamefanya kosa la kisheria."

No comments:

Post a Comment