Tuesday, January 30, 2018

RAILA ODINGA AJIAPISHA KUWA RAIS WA KENYA.



Raila aondoka uwanja wa Uhuru Park


Punde tu alipofika na 'kula kiapo' Raila Odinga ameondoka.
Wengi wamekuwa wakisubiri kwa hamu na ghamu, bila kutegemea kwamba atachukua muda mfupi hivyo.
Awali Raila Odinga aliiambia kituo cha habari cha KTN kwamba shughuli hio ' si mapinduzi ya serikali'
Raila 'akula kiapo'

Odinga akula kiapo uwanja wa Uhuru Park

Raila Odinga amefika katika pamoja na viongozi kadha wakuu wa NASA na kujiapisha akishika Biblia.
Amewaambia kuwa mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper ataapishwa baadaye.
Viongozi wengine wenza wa Nasa Moses Wetangula na Musalia Mudavadi pia hawakufika katika wuanja huo.
Bw Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya.
"Hatua ya leo ni kuelekea kutoa udikteta na kuleta demokrasia Kenya"
"Maelekezo mengine mtayapata baadae"

Bw Raila Odinga amezungumza na kituo cha habari cha KTN kwa njia ya simu ambapo amesisitiza kwamba Rais Uhuru Kenyatta hakuchaguliwa kwa njia halali.
Alipoulizwa anni atamwapisha, amesema: "Ngoja uone” na akasisitiza kwamba wanachokifanya leo kina msingi wake katika sheria na si mapinduzi.
“Hatutambui uchaguzi wa Oktoba 26 (uchaguzi wa marudio ambao Odinga alisusia), zaidi ya asilimia 86 ya Wakenya hawakushiriki. Tuna serikali ambayo si halali ambao inajidai kuwa mamlakani,” amesema.
Kuhusu taarifa kwamba amepokonywa walinzi, amesema: "Walinzi wangu waliondolewa muda mrefu sana uliopita. Najihisi kuwa hatarini ndio lakini watu raia ndio usalama wangu.”
Bw Odinga ameitaka serikali kutotumia nguvu kuusambaratisha mkutano wa leo.
"Wafuasi wangu wamo safarini kuelekea Canaan. Safari yetu ni halisi na haiwezi kuzuiwa.


  • Raila Odinga azungumza na vyombo vya habari dakika chache kabla ya kuelekea ‘kuapishwa’.
    Akizngumza kwa njia ya simu na kituo cha habari cha KTN, Odinga amesema kuwa hawakutarajia kufungwa kwa vyombo vya habari.
    Ni hali ya ‘kusikitisha’ na ‘inaonesha kuwa tumefika kiwango cha Uganda.'
    Alipoulizwa nani haswa atamuapisha, Odinga alijibu ‘ngoja uone.’
    Alielezea kuwa shughuli yao ni halali na haikiuki katiba. Pia amesema haamini kwamba wanachokifanya si mapinduzi ya serikali.

    No comments:

    Post a Comment