Monday, August 5, 2013

YANGA YATOA SALAAM LIGI KUU TZ BARA YAIBANJUA MTIBWA SUGAR 3-1 TAIFA.


  Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima (kulia) akiruka kukwepa kwanja la beki wa Mtibwa Sugar, Hassan Ramadan (katikati) wakati wa mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu kujiandaa na Ligi Kuu ya Tanzania Bara inayotarajia kuanza Agosti, 24, mwaka huu, ambapo pia ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Hisani katia ya Yanga na Azam, unaotarajia kupigwa mwezi huu. 
Katika mchezo huo Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 3-1, bao la kwanza la likifungwa na Said Bahanuzi katika dakika ya 26, bao la pili likifungwa na Jerry Tegete, kwa mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kuangushwa katika eneo la hatari katika dakika ya 81 huku hitimisho la mabao hayo likihitimishwa na Hussein Javu, katika dakika ya 87. 
Na bao la kufutia machozi la Mtibwa Sugar, lilifungwa na Shaaban Kisiga, kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 57.
.
 Kipa wa Mtibwa Sugar, akiokoa moja ya hatari langoni kwake.




 Wachezaji wa Mtibwa wakipita kuwasalimia wachezaji wa Yanga, kabla ya kuanza kwa mtanange huo.
 Kikosi cha Yanga kilichoanza.

No comments:

Post a Comment