Thursday, August 15, 2013

WANAWAKE WA KKKT WATAKA SERIKALI NA VIONGOZI WA KANISA KUPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA WATOTO CHINI YA MIAKA 12 KUPAMBIA HARUSI.

Katibu wa Idara ya Wanawake wa kanisa la kiinjili la kirutheli Tanzania Dayosisi ya Dodoma Mchungaji Sara Oforo Akifafanua jambo alipokuwa akiongea na viongozi wa ngazi mbalimbali wa idara hiyo walipokuwa kwenye tamasha la wanawake wa kanisa hilo mkoani hapa.
Muinjilist wa KKKT dayosisi ya Dodoma Daniel Kitua akiwaongoza akinamama wa kanisa hilo kuomba walipokuwa kwenye tamasha lililokutanisha wanawake wa kada mbalimbali kutoka wilaya za Mpwapwa, Kongwa, Konda na Dodoma Mjini iliyofanyika katika ukumbi wa Martin Ruther.
Wanawake wa kanisa la KKKT wakiomba kwa kuinua mikono wakati wa tamasha lao lililofanyika Dodoma 12, - 15. 08. 2013 huku kukiwa na masomo lukiki yakiwemo ya Haki ya mtoto, namna ya kuchangia Rasimu ya katiba, Ndoa na Maadili.
[PICHA NA JOHN BANDA]

Na John Banda, Dodoma
WANAWAKE wa kanisa la kiinjili la kiluther Tanzania wamewataka viongozi wa serekali na kanisa kutoa Adhabu kali kwa watu wanaotumia watoto walio chini ya maiaka 12 kupambia maharusi.
Wanawake hao wametoa Kauri hiyo walipokuwa kwenye Tamasha lao lililowakutasha  wakitokea Wilaya za Mpwapwa,Kongwa, Kondoa na Dodoma mjini huku wakiwa na mada za namna ya kuchangia Rasimu ya katiba, haki ya mtoto, maombi, Ndoa,maadili wosia na Sheria.
Mapaleshiweka Julieth Mapuga na Veroda Ngewe wa Dayosisi za Kondoa na Kibaigwa walisema watoto wa miaka nane na kumi wamekuwa wakiteseka sana kwenye kumbi za sherehe hasa za harusi na bila aibu wanaitwa Bibi na Bwana Harusi wadogo.
Mapuga alisema pamoja na kuona watoto hao wakipendezesha muonekano wa harusi kuanzia makanisani mpaka kwenye kumbi za sherehe jamii ijue inawachosha na kuwaharibu kisaikorojia kwa sababu ya mambo yanayofanyika kwenye ukumbi hizo ni ya kikubwa.
Aliongeza kuwa baada ya hapo watoto hao wanapokuwa kwenye michezo ya yao wanaiga na kuwa mke na mume huku wakiiga yote waliyoyaona kwenye kumbi, hali hiyo ni kinyume na haki za watoto hivyo viongozi wa serekali na kanisa wasaidiane kuwaelimisha wazazi na ikibidi wapewe adhabu kali.

“Ili kukomesha hali hii imefika wakati Serekali ichukue hatua kali za kisheria kwa sababu viongozi wa dini wanafundisha maadili lakini jamii imekuwa kama jiwe linalonyeshewa na mvua, pamoja na KKKT kupiga marufuka utumikishwaji wa watoto namna hiyo Adhabu kali zitolewe ili kuwanusuru watoto wetu’’, alisema Veroda Ngewe.
Kwa upande wake Katibu wa Idara ya Wanawake na Watoto Sara Oforo alisema somo kuhusu malezi ya watoto ni muhim kwa sababu maadili ya mtanzani yameporomoka kwa kiwango kikubwa.
Oforo alisema watoto wadogo wananyimwa haki zao kutokana wao hujifunza kwa kuona na kusikia hivyo wanapotumikishwa kwa jinsi hiyo pindi wanapokua kiasicha miaka 5 huanza kuiga yale ya kwenye harusi.
Aidha alisema pamoja na kanisa kuendelea Elimu kwa jamii husika ifike mahali serekali nayo iingilie kati kwa kota adhabu ili kulinusuru taifa tofauti na hivyo kusipokuwa na mkazo wowote taiafa linaelekea pa


No comments:

Post a Comment