Friday, August 16, 2013

MWENGE WA UHURU WAWASILI MKOANI DODOMA TAYARI KWA KUKIMBIZWA WILAYA ZOTE ZA MKOA HUO.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi a.k.a mtu wa mungu vanga likiwa limekolea akiserebuka pamoja na kikundi cha vijana cha hamasa kutoka Mkoa wa Dodoma wakati wa shamrashamra za kuupokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoa wa Singida leo hii.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi wakati wa sherehe za makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru baina ya Mikoa hiyo, makabidhiano hayo yamefanyika kijiji cha Mpendo Dodoma
Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa kutokea Mkoa wa Singida kwenda kukabidhiwa Mkoa wa Dodoma kwenye Kijiji cha Mpendo mapema leo hii.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kulia) akimkaribisha kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2013 Juma Ali Simai Mkoani Dodoma.
mkuu wa mkoa wa singida mh parseko kone na mkuu wa mkoa wa dodoma mh dr rehema nchimbi kabla ya makabidhiano ya mwenge wa uhuru.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akitoa salamu za Mkoa wakati wa Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Singida, sherehe hizo zilifanyika mapema leo hii kwenye kijiji cha Mpendo Dodoma. Kulia kwake ni kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2013 Juma Ali Simai.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Francis Isack (kulia) akiwa amepokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kushoto) tayari kwa kuukimbiza kwenye Wilaya ya Chemba leo hii.

No comments:

Post a Comment