Tuesday, August 20, 2013

MBIO ZA MWENGE ZAINGIA DOSARI MSAFARA WAPATA AJALI MBAYA MKOANI DODOMA JUMLA YA WATU 5 WAMEJERUHIWA VIBAYA.



MBIO za Mwenge wa Uhuru uliokuwa ukikimbizwa katika Wilaya ya Dodoma mjini zimeingia Dosari baada ya kupata ajali kilometa 3 kabla ya kukabidhiwa wiliya ya Mpwapwa.
Ajali hiyo iliyotokea jana majira ya 2;24 asubuhi katika mtelemko wa mlima fufu wilayani Chamwino na kusababisha watu 5 kujeruhiwa na kukimbizwa katika hospital ya mkoa wa dodoma.
Watu hao ambao majina yao Bado hayajatambulika walipata majeraha katika maeneo mbali mbali ya miili yao ikiwemo kichwani, kifuani, mguuni na mikononi.
Kaimu Kamanda wa polisi Suzan Kaganda aliyefika na kujione hali ilivyokuwa katika eneo hilo alisema chanzo cha ajali hiyo ni Matuta yaliwekwa kwenye Barabara hiyo inayojengwa kwa kiwango cha lami toka fufu hadi Dodoma bila kuwa na alama yoyote.
 majeruhi akisaidiwa kupekwa kwenye gari tayari kukimbizwa hospital
 gari iliyokuwa imembeba kiongozi wa mbio za mwenge ikiwa imeumia vibaya



 majeruhi wakipatiwa huduma ya kwanza kabla ya kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa dodoma kwa matibabu


 huduma ya kwanza
mama akisaikia naunivu nakali nguuni baada ya ajali.
PICHA NA JOHN BANDA

No comments:

Post a Comment