Thursday, August 15, 2013

ASKARI FEKI WA USALAMA BARABARANI ANASWA JIJINI DAR.



 ''RIAFANDE BANDIA RIKIWA CHINI YA ULINZI''.  Askari Bandia wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliyekamatwa leo mchana maeneo ya Kinyelezi Mnara, Tabata jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya sare zake, akiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa. Askari huyo feki amefikishwa kwenye Kituo cha Polisi Stakishari ili taratibu za kisheria ziweze kuchukua nafasi yake kwa udanganyifu huo aliokwisha ufanya na kujipatia pesa kwa madereva kibao.
Afande huyo aliyejipachika cheo cha Sajent, akiwa chini ya ulinzi wa Polisi mara baada ya kukamatwa mchana wa leo akila vichwa maeneo ya Kinyelezi Mnara,Tabata jijini Dar es Salaam.
Afande huyo akiwa Kituo cha Polisi Stakishari na sare zake kaaaama wenyeweeeee.

No comments:

Post a Comment