Tuesday, August 6, 2013

RAIS AMTEUA JAJI FRANCIS MUTUNGI KUWA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI

P 1
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Mh. Francis Mutungi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha majaji 10, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam mwaka jana. (Picha na Maktaba).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji Francis S.K.Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.
Taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Agosti 5, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita Agosti 2, 2013.
Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria.
Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM. 
5 Agosti, 2013

No comments:

Post a Comment