Thursday, August 29, 2013

KUFUNGWA KUBAYA SANA CHUJI AMFUATA MWAMUZI CHUMBANI KUTAKA KUMDUNDA KATIKA MCHEZO KATI YA YANGA NA COASTAL UNION.

Askari Polisi wakimzuia Kiungo Mkabaji wa Yanga, ambaye ni majeruhi, Athuman Idd 'Chuji' aliyechukizwa na uchezeshaji mbovu wa mwamuzi wa mchezo kati ya Yanga na Coastal, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, leo jioni. 

Chuji alikuwa akimsaka mwamuzi huyo ili kumtia adabu kutokana na maamuzi yake ya kuwapa penati wapinzani wao ambayo wao waliielezea kuwa haikuwa sahihi. Mwamuzi huyo Martin Saanya, alitoa penati katika dakika ya 90+ kwa kile kilichoonekana kuwa Beki wa Yanga David Luhende aliunawa mpira huo, huku mshika kibendera wake akiwa karibu kabisa na eneo la tukio na kushindwa kutoa maamuzi kwa kumsaidia mwamuzi wake ambaye alipuliza kipyenga cha kuashiria mkwaju wa penati hiyo iliyowakasilisha mashabiki na wachezaji wa Yanga.

Katika mchezo huo Yanga ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia mshambuliaji wake, Didier Kavumbagu, katika dakika ya 68, kufuatia pasi nzuri iliyopigwa na David Luhende, na Coastal, walisawazisha bao hilo kwa mkwaju huo wa penati uliopigwa na Jerry Santo.

No comments:

Post a Comment