Sunday, August 18, 2013

HURUMA WOMEN GROUP WAANZISHA MRADI WA BINTI SIMAMA IMARA ILI WASIJIINGIZE KWENYE NGONO KABLA YA MUDA.


 




Na John Banda, Dodoma 

ASASI ya Huruma Women Group isiyo ya Kibiashara inayojishughurisha na mradi wa Binti Simama imara imeanzisha mbinu mpya ya kuwajenga vijana wasijiingize kwenye ngono kabla ya muda kupitia Shule za Sekondari.
Mbinu hiyo waliyoanza nayo imezihusisha shule tano za sekondari za Mpunguzi, Makutupola, Miyuji, Hombolo na Dodoma zote zikiwa katika manispaa ya Dodoma.
Mwenyekiti wa Asasi hiyo Caroline Kisinza alisema pamoja na  kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwenye eneo la Elimu waliona hitaji hilo la kuwasaidia mabinti nao wajitambue.
 Kisinza alisema Lengo kubwa la mradi huo ni kuwawezesha vijana wakike  kupata elimu ya afya ya uzazi na makuzi, kutokana na kugungua kuwa vijana hao hawana mbinu za kujikinga na njia hatarishi zikiwemo ngono na madawa ya kulevya.
“Tuligundua kuwa vijana wengi wanakatizwa masoma kutokana na mimba zinasababishwa na ngono kabla ya wakati huku wengine wakijiingiza kwenye madawa ya kulevya kutokana na kutojitambua ndiyo maana tumeanzisha mradi huu wa Binti simama Imara’’, alisema Kisinza
Aidha alisema kwa kuanzia wameanza na wanafunzi Elfu mbili kutoka katika shule 5 wakike na wakiume kwa majaribio huku wakiwa na matarajio kuwa mradi huo utafanikiwa kutokana na kuwalenga wahusika moja kwa moja.
Kwa upande wake Mratibu mwandamizi wa Shirika la Social Action Trast Fund [SATF] wanaofadhili mradi huo Nelson Rutabanzibwa alisema mwishoni mwa mwaka watafanya tathimini na kama kutakuwa na mafanikio watausambaza mradi huo nchi nzima.
Rutabanzibwa aliongeza kuwa pamaoja na tatizo la ngono za mapema kuwa mashuleni Bado pia ni jukumu la jamii husika kutokana na kuwa walimu wanalalamika kuwa wanafunzi wengi hugundulika wana mimba hasa wanapotoka likizo za masomo.
Alitanabaisha kuwa wanampango wa kuifuata jamii ili kuipa elimu hiyo ili kuwanusuru mabinti na janga hilo la ngono kabla ya wakati kutokana na kutojitambua kwa vijana hao na jamii yenyewe ili kuondoa tatizo pande zote mbili.

Mgongano huo wa mawazo ni muendelezo wa Mradi wa Binti simama imara uliojumuisha wanafunzi 2000  ulihusisha jumla ya shule tano za sekondari za manispaa ya Dodoma za mpunguzi,makutupola, miyuji, hombolo na Dodoma Sekondari.

No comments:

Post a Comment