Saturday, August 17, 2013

Huruma Women Group yaanza kampeni ya kuzuia ngono kabla ya wakati.

Mratibu Mwandamizi wa shirika lisilo la kiserekali la Social Action Trast Fund [SATF] Nelson Rutabanzibwa akifafanua jambo alipokuwa akifungua Malumbano ya hoja kwa wananafunzi wa Shule za Sekondari za Miyuji, Makutupora na Hombolo, Mada ikiwa Umasikini ni chanzo cha vijana wengi kujihusisha na Ngono kabla ya wakati.
Mwanadada Mkeleketwa wa Umasikini kuwa siyo chanzo cha Ngono kwa vijana Simfya akizungumza kwa jazba alipokuwa akichangia Mada hiyo.
Mratibu Mwandamizi wa SATF Nelson Rutabanzibwa akifafanua Jambo wakati alipokuwa akiwapongeza wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Hombolo kutokana na kuigiza kwa ufanisi igizo lililoonyesha makundi kuwa chanzo cha mimba na kufukuzwa shule.
Ofisa wa kujitolea katika Utekelezaji wa Mradi wa Asasi ya Huruma Women Group [HWG] Anjelo Lukas akichangia wakati Malumbano ya hoja juu ya umasikini kuwa chanzo cha vijana wengi kujiingiza kwe ngono kabla ya wakati.
Walimu wa Shule hizo waliohuzuria Ukumbini hapo Waifuatili wakifuatilia kwa karibu michango mbali mbali ya  wanafunzi kwenye mgongano huo wa mawazo ambapo mengi yalichangiwa kuhusu umasikini kuwa chanzo cha vijana wengi kujiingiza kwenye ngono mapema.
Makundi haya ya wanafunzi wakiingia kwenye ukumbi wa Dodoma Sekondari walipohudhuria mgongano wa mawazo kuhusu umasiki kuwa chanzo cha Ngono za mapema kwa vijana, ulioandaliwa na Asasi ya Huruma Women Group chini ya Social Action Trast Fund inayojihusisha na Mradi wa Binti Simama Imara.
[PICHA NA JAHN BANDA]

No comments:

Post a Comment