Saturday, August 10, 2013

FRANCIS MIYEYUSHO AMKALISHA MZAMBIA RAUNDI YA NANE, KIDO AKALISHWA RAUNDI YA KWANZA


Bondia Fidelis Lipupa wa Zambia akiwa chini akitafakari kuendelea kusulubiwa katika pambano hilo ama la, baada ya kukalishwa na mpinzani wake Francis Miyeyusho wakati wa pambano lao la Kimataifa lililofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Dar es salaam, jana usiku. Miyeyusho alishinda kwa K,o ya raundi ya nane Picha na SUPER D


Bondia Mtanzania Francis Miyeyusho (kulia)  akipambana na Fidelis Lipupa wa Zambia wakati wa  mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika wakati wa Sikuku ya Iddi katika ukumbi wa Dar Live jana.
Mwamuzi wa pambano hilo akimhesabia Bondia Lipupa wa Zambia, baada kukalishwa na Miyeyusho, katika Raundi ya Nane..

Myeyusho, akishangilia ushindi na mashabiki wake, baada ya kutangazwa kidume katika pambano hilo.

No comments:

Post a Comment