Monday, September 2, 2013

MBUNGE WA DODOMA MJINI BW DR DAVID MALOLE AJITOA RASMI CDA.



Na John Banda, Dodoma
MBUNGE wa Dodoma Mjini Mhe, Dkt. David Malole amejitoa Rasmi
kujihusisha na Bodi ya mamlaka ya ustawishaji makao makuu [CDA]
kutokana na kutoshirikishwa katika maamuzi mbalimbali.
Mbunge huyo alichukua uamuzi huo wakati alipofika kujionea bomoabomoa
iliyofanywa na mamraka hiyo, baada ya kubomoa vibanda vya makumbusho
ya wagogo vilivyopo mlima Bwibwi.
Dkt. Malole alisema Hawezi kuendelea kujiona mjumbe katika bodi hiyo
wakati hashirikishwi kwenye maamuzi mbalimbali yakiwemo ya upangaji wa
mji huo na kubwa zaidi wakati mamraka hiyo inapopanga kwenda kubomoa
nyumba za watu.
Aliongeza kuwa yeye kama mbunge na aliyechaguliwa na wananchi Hawezi
kuendelea kuvumilia kuona  wakionewa kwa kufanyiwavitendo vya kinyama
vya kuvunjiwa tena hata bila ya kusikilizwa.
“Mimi kama mjumbe wa Bodi ya CDA, Sijashirikishwa hivyo nakubaliana na
hoja za wananchi wanazosema kuwa watendaji wa mamraka hiyo akiwemo
mkurugenzi wananidharau,
“Mahudhurio yangu kama mjumbe kwenye bodi hayana maana yoyote nikienda
sithaminiwi , hivyo kuanzia leo najitoa, Siwezi kuendelea kuwa mjumbe
wa Bodi ambayo inanyanyasa wananchi’’, alisema Malole
Aidha Dkt Malole alisema yeye kama mbunge CDA haifai na kuishauri
serekali kuwa ni afadhali majukumu waliyopewa mamraka hiyo yahamishiwe
Halimashari ya manispaa hiyo ambayo inaweza kutekeleza majukumu hayo
bila kubuguzi wananchi wake.

Mwenyekiti wa kijiji hicho cha makumbusho ya kimila cha Bwibwi [Mzenga
itumbi] Andason Chaulema alisema wafanyakazi wa CDA walifika katika
eneo hilo palipo na Kisima cha maajabu wakiwa na Tinga tinga, huku
wakiwa na polisi zaidi ya 10 na walipofika waliiga risasi 3 hewani.
Chaulema alisema baada ya watu kutawanyika kukimbilia mapolini yeye
alibaki kuwasikiliza baada ya kuona wapo na watu wa CDA, wakmuuliza
kibali cha kujenga nyumba za makumbusho hayo aliposema wamsubili Mtemi
wao Lazaro Chihoma wakakataa na kuanza kubomoa nyumba hizo
zilizojengwa kwa miti  juu na chini.
Nao viongozi wa Chama cha mapindizi [CCM] wilaya ya Dodoma mjini
Katibu Mwenezi Wilaya Salum Kalli na Mjumbe wa kamati ya Siasa [W] CCM
Judith Myeya walisema kuhifadhi makumbusho ya kimila ni sera ya chama
hicho iliyopo kwenye ilani ya 2010/15.
Kalli aliongeza  kuwa vitendo hivyo vinavyofanywa na CDA ni vya
kukidharirisha  na kukiondolea chama imani kwa wananchi wake na
kuahidi kulifikisha kwa mwenyekiti  Jakaya Kikwete ili aiangalie upya
mamraka hiyo kama ina haja ya kuendelea kuwepo la sivyo watawashawishi
wananchi ili wapige kura za maoni ili kuikaa.
Kisima cha maajabu kilichopo katika Mlima huo wa Bwibwi kilivumbuliwa
na Mbwa aliyekuwa na kiu ya maji aliyemtoroka muwindaji [Mpelembi]
aliyekuwa akiwinda pembezoni mwa mlima huo miaka ya 1850 na kutawazwa
kuwa mtemi wa kitongoji hicho baada ya kuhamia kutoka na kupata maji
yaliyowasaidi watu wa kipindi hich


Mjumbe wa Kamati ya siasa CCM Wilaya ya Dodoma Judith Myeya akifafanua
jambo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mala baada ya kujionea
jinsi makumbusho ya kimila ya kabila la kigogo yalivyobomolewa na
Mamlaka ya ustawishaji makao makuu CDA, na kupendekeza mamlaka hiyo
ifutwe.


Mbuge wa Dodoma Mjini DKT David Malole ambae ni mjumbe wa Bodi ya CDA
akionyeshwa miti na mabaki mengine na Mtemi Lazaro Chihoma namna
makumbusho hayo ya kimila yaliyojengwa katika mlima wa Bwibwi
yalivyobomolewa na CDA.


Chief Lazaro chihoma [katikati] akiwaongoza Mbunge wa jimbo la Dodoma
mjini DKT David Malole, Katibu Mwenezi wa CCM wilaya Salum Kalli,
mjumbe wa ya siasa wa wilaya CCM Judith Myeya na viongozi wengine
kuona sehemu ya ikulu ya kimila ilivyohalibiwa na CDA.


Wananchi wa kijiji cha iyumbu wakiwa wamejiinamia wasijue la kufanya
baada ya tinga tinga la CDA kufika na kubomoa Makumbusho ya kimila
yaliyojengwa katika mlima wa Bwibwi chini ya ulinzi mkali wa polisi
mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment