Saturday, September 7, 2013

MOTO MKUBWA WAZUKA MSIKITI WA MANYEMA MJINI DODOMA.

Na John Banda, Dodoma
MOTO mkubwa umezuka katika msikiti wa manyema uliopo barabara ya saba manispaa ya Dodoma na kusababisha uaharibifu wa sehemu ya jingo hilo pamoja na samani mbalimbali.
Mashuhuda wa Tukio hilo waliuambia mtandao huu kuwa baada ya kuswali swala ya ijumaa na kuondoka walishtukia moshi mkubwau kisambaa kutokea juu ya msikiti huo.
 Walisema baada ya kuona hivyo waliamua kuwajulisha kikosi cha zimamoto kwa kutumia simu zao na baada ya muda mfupi walifika na kuanza kuzima Moto huo uliokuwa ukisambaa kwa kasi kuanzia juu ya gholofa ya msikiti huo.
 Mmoja waumini hao alietambulika kwa jina moja la Said alisema waliona moto huo ukianzia juu  kwenye maungio ya Umeme sehehemu ya men swichi ambapo uliendelea kusambaa kabla ya kudhibitiwa na kikosi cha zimamoto
Kamanda wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Dodoma Damas Nyanda aliyefika na kujionea hali halisi alisema walikuwa bado hawajapata taarifa kama kulikuwa na mtu yeyete aliyejeruhiwa ama kupoteza maisha.
Alisema mpaka wakati huo walikuwa wanaendele na zoezi la uokoaji na baada ya mambo yate kuhakikiwa taarifa rasmi ya hasa iliyopatikana baada ya tahimini ya viongozi wa msikiti huo.
Kwa upande wake mkuu wa kikosi cha zimamoto mkoa Sajenti Amiry Issa alisema walifika Dakika 4 baada ya kupokea Taarifa ya ajali hiyo ya Moto na kukuta moto umesamba maeneo mbalimbali ya msikiti huo wenye gholofa moja.
Issa alisema urahisi wa kuzima moto huo ulitokana na wao kupewa taarifa mapema kabla ya moto kusambaa sana na kuwa na madhara makubwa.
Akatumia Fursa hiyo kuwataka watu kutofanya juhudi za kuzima mioto yoyote inayojitokeza wenyewe kabla ya kuwajulisha zimamoto maana kwa kufanya hivyo kunachelewesha uzimaji na kusababisha hasara kubwa
mtandao huu ulishuhudia Mazuria yanayotumiwa kuswali, vitabu, kanzu na nafaka iliyokuwa Ghorofa ya juu kuwa imeunguzwa na moto huo uliozuka kuanzia majira ya saa 8. 10 mchana.


Moshi mkubwa ukitoka katika sehemu ya msikiti wa Manyema  uliopo Barabara ya Saba Dodoma, amba po chanzo cha moto huo ni Hitilafu ya umeme.

Waumini wa Msikiti huo wakisukuma maji yaliyotumika kuzima moto uliokuwa umeshika katika msikiti huo baada ya Hitilafu ya umeme na kusababisha hasara kubwa.
 Waumini wa Msikiti wa Manyema uliopo Barabara ya Saba Dodoma wakiangalia mabaki ya samani za msikiti huo ulioshika moto ambapo chanzo chake kinadaiwa kuwa hitilafu ya umeme.

wakitoa mazuria yanayotumiwa katika swala mbalimbali na waumini wa msitiki wa Manyema baada ya kuunguzwa na moto uliosababishwa na Hitilafu ya umeme.

No comments:

Post a Comment