Tuesday, September 24, 2013

AJALI MBAYA SANA DODOMA, BASI LA AL-SAYD LAGONGANA USO KWA USO NA LORI NA KUUA WATU 6 PAPO HAPO

 
Na John Banda, Dodoma
MWENDO kasi wa speed 140 aliyokuwa akiutumia Dereva wa Basi la Al sayd Expess umesabisha vifo vya zaidi ya watu 6 akiwemo yeye na dereva wa lori alilogongana nalo na wengine 17 kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa .
Ajali hiyo iliyotokea katika kijiji cha chinangali 2  wilayani Chamwino mkoani Dodoma wakati basi hilo lenye namba za usajili T 433 DLR  lililokuwa likitokea Dar es saam  kuja mkoani hapa lilipogongana uso kwa uso na lori hilo lenye namba za usajili T102 CGR aina ya Layland Daf lilikuwa na tera.
moja wa majeruhi wa ajali hiyo Juma Yusuph 31 mhehe  mkazi wa Chidachi manispaa ya Dodoma alisema mwendo huo ulibadilika na kuwa mkubwa kuanzi walipotoka mkaoni Morogoro kiasi cha kufikia kasi hiyo.
‘’Mimi nilikuwa nimekaa mbele karibu na dereva nilipochungulia nikaona  speed inasoma 140 huku jamaa akiyapita magali ya mizigo zaidi ya 4 kwa pamoja kama unavyoona mimi nimevunjika mguu lakini siwezi kusema moja kwa moja kuwa Yule dereva ni kama alipanga kujiua na kweli nilishuhudia baadhi ya viungo vyake mbele ya lori’’, alisema yusuph.
Majeruhi wa ajali hiyo ambao wengi wao walivunjika viungo vikiwemo miguu na mikono walisema mwendo mkubwa uloanza baada ya kutoka  Morogoro
Kaimu kamanda wa polisi mkoa Damas Nyanda aliwataja majina waliopoteza maisha mbele ya  wandishi wa habari kuwa Dereva wa lori Hassan Mohamed umri kati ya 30,35, Ahmed Said, Husen Rajab, Imran Sharif wakazi wa Dar, na Dereva wa Basi hilo Nizar Akran Khan mkazi wa Mpwapwa  wakati mwili wa marehemu mmoja bado haujatambuliwa.
Kaimu kamanda huyo alisema Alisema Miili ya maremu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma na wengine 17 waliojeruhiwa kulazwa wakiwemo 7 wanawake na wanaume 10
Nyanda  alisema chanzo cha ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 2.30 usiku wa juzi  jumapili  ni Mwendo kasi wa Dereva wa Basi hilo ambapo ashindwa kulimudu wakati akijaribu kusimama ili kujaribu  kujiepusha na ajali hiyo.
Jeshi hilo la polisilimetoa wito kwa watumiaji wa barabara kuwa waangalifu wanapokuwa barabarani huku wakiwa natahadhali ya kujua kuwa kuna watumiaji wengine.
 

Daktari wa Mifipa wa hospital ya Rufaa ya Dodoma Maitundo Stanley akimhudumia mmoja wa majeruhi  wa ajali iliyohusisha Basi la Al sayed lililokuwa likitoka Dar es  laam kwenda Dodoma na Lori la mizigo uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu 6.

 
Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Damas Nyanda akitoa ufafanuzi kuhusu ajali iliyohusisha basi la Al sayed na Lori la mizigo na kusababisha vifo vya watu 6 na wengine 17 kujeruhiwa vibaya ikiwemo kuvunjika viungo mbalimbali vya miili yao.

Askari wa kikosi cha usalama Barabarani akichukua maelezo kwa mmoja wa majeruhi wa basi la al sayd express lenye namba za usajili T433 BLR lililogangana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba mahindi kupeleka Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment