Friday, September 20, 2013

KIJIJI CHA SEGERA, CHAMWINO MKOANI DODOMA HAWANA MAWASILIANO YA SIMU.


Na John Banda, Chamwino
WAKAZI wa kata ya Segara Wilayani Chamwino mkoani Dodoma wamelalamikia kukosekana kwa huduma ya mawasiliano hali inayowafanya kukosa huduma za msingi kwa wakati ikiwemo kuuza mazao kwa bei yahasara.
Wakazi hao waliitoa kauli hiyo katika kijiji cha Malechala walipokuwa kwenye Tambiko la kimila lilihudhuliwa na makabila mbalimbali yaliyoongozwa na Wanguu toka mkoani Tanga lililohudhuriwa na watu zaidi ya 400 na kufanyika katika himaya ya Fundi  Shabani Waziri  mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho Asha Mohamed   alisema kumekuwa na kelo ya ukosefu wa mitandao ya mawasiliano tangu ilipoanzishwa hapa nchini hali ambayo imekuwa ikiwasababishia kukosa kila huduma za kijamii kwa wakati.
Alisema kutokana na kata hiyo kuwa mbali na makao makuu ya wilaya hiyo ya Chamwino wamekuwa wakipata taabu ya utoaji wa taarifa za matukio mbalimbali zikiwemo za ajali, ujambazi, wizi, wagonjwa wanaohitaji huduma za haraka pia wameshindwa kujua wakati mzuri bei za mazao.


Mwanamama ambaye hakufahamika jina akiwa ndani ya shimo huku akielekezewa Damu ya mbuzi aliyekatwa shingo wakati alipokuwa akipata moja ya tiba zinazotolewa nyumbani kwa mzee Shabani Waziri aliyeamua kuijenga nyumba hiyo katikati ya poli na umbali wa kuingia kijiji cha Malecela km 2 .
Kiongozi wa waganga wa tiba za jadi  Fundi Shabani Waziri akimshika mmoja wa waganga waliohuzuria tambiko hilo kama ishara ya salamu zinazotumika wakati wa tambiko.
Mgeni Rasmi katika tambiko hilo Fundi mkuu wa waganga wa tiba za jadi Sangali Chambo akimuwekea mkono  Kiongozi wa waganga hao Shabani Waziri kama kielelezo cha salamu za heshima wakati wa tambiko hilo lilifanyika katika himaya yake kwenye nyumba iliyopo umbali wa zaidi ya km 2 toka kijiji cha Malecela.

No comments:

Post a Comment