Friday, February 8, 2013

MELI YA MV VICTORIA ILIVYNUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO

Maofisa wa kikosi cha zima moto wakijitahidi kuzima moto uliokuwa tayari umesambaa katika maeneo ya Meli ya Mv Victoria ambapo walifanikiwa kuuzima huku ukiwa tayari umeteketeza magodoro yote pamoja na mito ya makochi iliyokuwa katika chumba cha kuhifadhia mizigo.

Meli ya Mv Victoria inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za Meli nchini (MSC) leo imenusurika kuteketea kwa moto uliozuka wakati mafundi wa kampuni hiyo wakichomelea eneo la shimo la kuhifadhia mizigo la mojawapo ya maeneo kwenye Meli hiyo.

Moto huo uliozuka katika meli hiyo ulizua tafrani kwa wakazi wa jiji la Mwanza na kusambaa katika eneo la maegesho ya Meli za Kampuni ya hiyo yaliyopo katika bandari ya Mwanza na kusababisha msongamano mkubwa katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment