Tuesday, February 12, 2013

*CCM YATEUA MAJINA YA WAJUMBE 14 WA KAMATI KUU CCM TAIFA MJINI DODOMA


Mwenyekiti-wa-CCM-Taifa-Rais-Jakaya-Kikwete.

Katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi kilichofanyika mjini Dodoma kwa siku mbili kuanzia 
Februari 10 na 11, 2013, pamoja na kuzungumzia mambo mengine kimeridhia kufanya uteuzi na kufanya uchaguzi wa 
Wajumbe 14 wa Kamati Kuu ya CCM.

Katika Kikao hicho Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imeridhia kuteuliwa kwa Dkt. Salim Ahmed Salim, ambaye 
ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu kupitia nafasi 10 za uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM, Dkt.  Jakaya Mrisho 
Kikwete.

Wajumbe 14 waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni:-
WAJUMBE WA KAMATI KUU TANZANIA BARA.
1. Ndugu Pindi Chana
2. Ndugu Adam Kimbisa
3. Ndugu William Lukuvi
4. Dokta Emmanuel Nchimbi
5. Ndugu Jerry Slaa
6. Profesa Anna Tibaijuka
7. Ndugu Stephen Wassira
WAJUMBE WA KAMATI KUU-ZANZIBAR.
1. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
2. Ndugu Hussein Mwinyi
3. Profesa Makame Mbarawa Mnyaa
4. Dokta Salim Ahmed Salim
5. Ndugu Maua Daftari.
6. Ndugu Samia Suluhu Hassan
7. Ndugu Hadija H. Aboud

No comments:

Post a Comment