Friday, February 8, 2013

ASKOFU THOMAS LAIZER WA KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI KATI AFARIKI

 Habari zilizoufikia mTANDAO HUU hivi punde kutoka Jijini Arusha zinaTAarifu kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Ask Thomas Laizer, PICHANI  amefariki dunia.

Imeelezwa kuwa  Askofu. Laizer amefikwa na umauti alasiri ya jana katika Hospitali ya Rufaa ya Selelian ya jijini Arusha.
 Februari 6, 2013 Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alimtembelea  na kumjulia hali Askofu Thomas Laizer wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati.
Taarifa zilipasha kuwa Askofu Laizer alilazwa Hospitalini hapo kwa zaidi ya mwezi mmoja, na hakuna daktari wala ndugu aliye tayari kusema ugonjwa unaomsibu.
Pinda alikwenda hospitalini hapo jana saa 9 alasiri na kukaa zaidi ya nusu saa, huku waandishi wa habari wakizuiwa kuingia katika chumba alimolazwa cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.
Hata hivyo, baada ya kutoka katika chumba hicho kama ilivyo ada ya viongozi kuzungumzia hali ya mgonjwa, Pinda hakuzungumza na waandishi wa habari na kulikuwa na ulinzi mkali ambapo pia waandishi wa habari walizuiwa kuzungumza naye.
Awali ilisemekana kuwa Askofu Laizer amehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya Moshi mkoani Kilimanjaro, baada ya watu wengi kumiminika Selian kutaka kumwona, lakini jana ilidhihirika kuwa, amelazwa hospitalini hapo.
 FK Blog inatoa pole kwa Waumini na washarika wote wa KKKT nchini kote kufuatia msiba huo mzito ulilolikumba Kanisa la Kilutheri hasa wakati huu ambao kuna mgongano kati ya waumini na Viongozi wa Dayosisi ya Kaskazini Kati.

No comments:

Post a Comment