Friday, February 1, 2013

KINANA ASHIRIKI KAZI ZA KIJAMII KIBONDO

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Kumwambo, Wilayani Kibondo, Jana, baada ya kushiriki ujenzi wa chumba cha darasa, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Kijiji cha Bunyambo Wilayani Kibondo, Jana, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. Wengine ni baadhi ya viongozi na wananchi aliofuatana nao kwenye msafara wake. 
 Baadhi ya wazee, watendaji na wajumbe wa mashina wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (hayupo pichani) alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Maendeleo wa Kibondo, Jana, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake tanganyika mjini Kigoma.

No comments:

Post a Comment