Friday, January 25, 2013

SIMBA YA OMAN YAIOGOPA BLACK LEOPARD YAINGIZA KIKOSI CHA PILI NA KUPOKEA KIPIGO KIKALI

Baada ya kipigo cha mara mbili mfululizo kutoka kwa timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, timu ya Black Leopards ya nchini Afrika ya Kusini, leo imepunguza machungu yake kwa kuichapa Simba ya jijini Dar es Salaam kwa bao 1-0, katika mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Hata hivyo imeelezwa kuwa kutokana na hofu Klabu ya Simba iliwachezesha wachezaji wa timu B, jambo ambalo limewakera hadi mashabiki wa Simba waliokuwapo uwanjani hapo leo, ambapo baadhi ya mashabiki waliohudhuria mtanange huo uwanjani hapo walisikika wakilalama kwa kitendo hicho, ambacho kimeelezwa kuwa ni sehemu ya hofu na dharau.

Katika Kikosi cha simba wameonekana wachezaji wanne tu walio katika kikosi cha kwanza cha ligi kuu. huku wachezaji wote waliobaki wakiwa ni wa kikosi cha pili, ambao wengi wao wakiwa ni watoto

No comments:

Post a Comment