Monday, January 28, 2013

KINANA NA MSAFARA WAKE WAKAGUA MATENGENEZO YA UWANJA WA NDEGE WA KIGOMA


Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, ukiingiwa kwenye eneo la Uwanja wa Ndege wa Kigoma uliopo eneo la Kipampa, kwa ajili ya kushuhudia maendeleo yaliyofikiwa katika ujenzi mkubwa wa kiwanja hicho unaoendelea ili kukiongezea uwezo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia wafanyakazi kwenye uwanja huo alipowasili.
Meneja wa Uwanja huo, Elipind Tesha (kulia) akimweleza  Kinana na ujumbe wake hatua ilipofikiwa katika ujenzi huu, ambapo alisema, umefikia asilimia tisini, na kwamba unaweza ingawa unaweza kuanza kutumika rasmi Aprili mwaka huu, lakini matengenezo yote yatakuwa yamekamilika Juni 2013. Wengine kutoka kushgoto ni, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Martin Shigela.
Kinana akimsikilliza Mhandisi Mkazi wa Uwanja huo,Cleopa Mpembeni (wapili kulia) akimpa maelezo ya kiufundi kuhusu ujenzi unavyoendelea.

No comments:

Post a Comment