Thursday, January 24, 2013

HIII NDIO YANGAAAAAAAAAAA



 
Golikipa wa timu ya Black Leopards, Posnett Omony, akisota kuokoa mpira uliotinga wavuni kutoka kwa mchezaji wa timu ya Yanga, Jerry Tegete, kwa njia ya penati.Timu ya Yanga imeibuka kidedea kwa kuinyuka Black Leopards mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa leo jioni kwenye Uwaja wa CCM Kirumba. Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Said Bahanuzi.
 Wachezaji wa timu Yanga wakishangilia bao la pili lililofungwa na Jerry Tegete, katika  kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati.
Mchezaji wa wa timu ya Yanga David Luhende (kulia) akipiga krosi huku Moses Kwena wa Black Leopards, akijaribu  kumdhibito wakatia wa mchezo huo uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
 Pichani ni Golikipa wa Black Leopards Posnett Omony akijitahidi kuokoa mpira uliopigwa kwa kichwa na mchezaji wa Yanga,Said Bahanuzi na hatimaye kutinga kimiani na kuandika bao la kwanza.

No comments:

Post a Comment