Saturday, January 5, 2013

MKE WA MAKAMU WA RAIS, MAMA ASHA BILAL MGENI RASMI MAHAFALI YA KIDATO CHA SITA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA KIISLAMU WA SHULE YA SEKONDARI TAMBAZA

 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake Mama Asha amewahasa vijana hususan wanafunzi hao waliohitimu masomo kutokukubali kutumika na watu wenye maslahi binafsi na kujikuwa wakisababisha uvunjifu wa amani. Aidha amewataka kutojihusisha na makundi yanayochochea uvunjifu wa amani bila kujitambua wafanyalo, badala yake amewambo kuwa wakipima kila wanaloambiwa kuwa linamaslahi na dini yao ama maslahi kwa jamii na taifa kwa ujumla. 
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita, Latifah Nuhu, wakati wa sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam. 
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita, Mwinga Gwao, wakati wa sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment