Saturday, January 11, 2014

WAKUU WA IDARA MBALIMBALI WILAYANI KONDOA WAPEWA MTIHANI MAALUMU WA KUPIMA UWEZO WAO KATIKA KUFUATILIA MASUALA YA WANANCHI.

Wakuu wa idara mbalimbali wilayani kondoa wakijitahidi kujibu mtihani uliotolewa Jana na mkuu wa mkoa wa dodoma (hayupo pichani) wenye lengo la kupima kiwango cha ufuatiliaji wa mambo na utendaji wa viongozi ngazi mbalimbali wilayani kondoa kuanzia watendaji kata, maafisa tarafa Wakuu wa idara mpaka mkuu wa wilaya hiyo.

Mkuu wa wilaya ya kondoa Omary Kwaangw' (kulia) akiumiza kichwa kutafuta majibu ya mtihani uliotolewa na mkuu wa mkoa wa dodoma Dr. Rehema nchimbi (watatu kutoka kulia) ill kupima kiwango cha ufuatiliaji wa mambo na utendaji wa viongozi wa wilayani kondoa.zoezi hili litafanyika kwenye wilaya ya zote za mkoa wa dodoma
Mbunge wa kondoa kaskazini Mhe Zabein Mhita akichangia hoja juu ya tathimini ya ufuatiliaji wa mambo na  utendaji wa viongozi na watendaji  wa serikali wilayani kondoa jana, katikati ni katibu tawala msaidizi anayeshughulikia serikali za mitaa Dodoma Ndg. Emanuel kuboja na kulia ni mkuu wa mkoa wa dodoma Dr Rehema nchimbi.

No comments:

Post a Comment