Monday, January 6, 2014

HUKUMU YA ZITTO KABWE YAPIGWA KALENDA MPAKA KESHO SAA NANE MCHANA.

Habari zilizoufikia mtandao huu hivi punde kutoka Mahakama Kuu,  zinasema kuwa Mahakama Kuu imeahirisha hukumu ya Zitto Kabwe dhidi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, ambayo ilikuwa imepangwa kutolewa leo asubuhi. 

Kwa maamuzi hayo ya Mahakama ya kuahirisha hukumu,  yalionekana kuwakera pande zote mbili wafuasi wa Zitto na viongozi wengine wa Chadema.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kwa watu waliokuwa mahakamani hapo, kesi hiyo sasa hukumu yake itasomwa kesho saa nane mchana. Kesi hiyo ni mwendelezo wa mgogoro mkubwa wa ulio ndani ya Chadema dhidi ya Kabwe anayedai kuwa hiyo ni vita ya ukombozi dhidi ya wahafidhina kwenye chama chao.

Jana katika mitandao ya kijamii walikuwa wakirushiana makombora ambapo Zitto alionekana kumjibu Tundu Lissu kama ifuatavyo.

"Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. Naamini Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini.

Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa. Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa.
Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni. Lissu anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka Conservative Party?

Nimefanya internship yangu kwa Mkono and Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda.

Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote. Lissu ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club Bilicanas.
They must know I am not a push over. Chacha died, I won't. Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake aliyemzaliwa mtoto hawezi kunmyooshea mtu kidole kuhusu maadili.

No comments:

Post a Comment