Saturday, February 1, 2014

ASKARI WATANO WAFA AJALINI PAPO HAPO BAADA YA GARI LAO KUGONGANA NA BASI LA MOHMED TRANSI ENEO LA MTUMBA MKOANI DODOMA


Na John Banda, Dodoma
 
ASIKARI Polisi watano mkoani dodoma wafariki dunia papohapo katika ajali ya gari iliyohusisha Busi Gari Ndogo.
Ajali hiyo iliyotokea jana majira ya saa 5.45 usiku katika kijiji cha mtumba wakati basi la kampuni ya Mohamed trans T 997 AVW lililokuwa likitokea Dar es laam kwenda Dodoma lililogongana na Toyota Corolla t 770 ABT
Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime alisema ajali hiyo ilisababisha vifo vya asikari polisi 5 wanaofanyia kazi wilayani kongwa ambao kwa pamoja walikuwa wakitokea kwenye sherehe ya kuwaaga wastaafu wa jeshi hilo iliyofanyikia Chuo cha Mipango.
Alisema ajali hiyo ilisababishwa na mwendo kasi ya madereva wote wawili hali iliyosababisha mburuzo wa zaidi mita 150 tokea yalipogongana.
Misime aliwataja askari hao waliopoteza maisha kuwa ni
1.           D.9084 D/CPL. ADOLF S/O MESHACK SILLA mwenye miaka 51, Mgogo.
2.           F.6459 D/C. EVARIST s/o MOSES BUKOMBE mwenye miaka 34, Muha.
3.           H.3783 PC. DEOGRATIUS s/o PATRICK MAHINYILA mwenyw miaka 29, Mgogo.
4.           WP.10337 PC. JACKLINE d/o AUGUSTINE TESHA mwenye miaka 22, Mchaga.
5.           WP.10382 PC. JEMA d/o JIMMY LUVINGA mwenye miaka 20, Mhehe. Wote ni askari Polisi Wilaya ya Kongwa na hakuna abiria aliyeumia katika basi.

Wito kwa madereva kila mara wawe na udereva wa tahadhari na kuzingatia sheria za usalama barabarani kutokana na ajali au kifo hakiangalii ni askari au mtu gani.
 GARI AINA YA TOYOTA COROLLA T770 ABT WALIOKUWEMO ASKARI HAO WATANO NA KUPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI HIYO
 HAPA GARI IKIWA TAYARI NJE YA KITUO CHA POLISI DODOMA IKIWA IMEHARUBIKA VIBAYA.
HII NDIO SURA YA GARI HIYO ALIYOSABABISHA VIFO VYA ASKARI 5 DODOMA IKIONEKANA KWA MBELE BAADA YA KUPATA AJALI.

No comments:

Post a Comment