Monday, February 3, 2014

MIAKA 37 YA CCM DODOMA MJUMBE WA NEC CCM ATAKA WANANCHI WAIKATE CDA.

Na John Banda,Dodoma.
BAADA ya hivi karibuni Mbuge wa jimbo la Dodoma mjini Dkt David Malole kutangaza kujitoa kwenye bodi ya CDA, Nae Mjumbe wa NEC ya chama cha mapinduzi [CCM] Anthony Kanyama agongelea msumali wa moto

Mnec Huyo aliugongomelea msumari huo wa moto baada ya kuwataka  Madiwani  wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuikataa Rasimu ya Muswada wa Sheria ya kutaka Mamlaka ya ustawishaji Makao Makuu (CDA) iendelee kuwepo.

Agizo hilo alilitoa kwenye  Maadhimisho  ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Kitongoji cha Mji Mwema Kata ya Chang’ombe Manispaa ya Dodoma .

Kanyama aliwataka kupinga suala hilo na kudai kuwa  Mamlaka hiyo tayari imeshaandaa  rasimu ya Muswada wa Sheria yenye mapendekezo yake ya kutaka kuendelea na wanataka kupeleka Bungeni ili uweze kusomwa licha ya wabunge na madiwani  ambao ndio walengwa kutoshirikishwa.

Alisema pamoja na wabunge na madiwani kuwa ndio wahusika wakuu, cha kushangaza hawakushirikishwa na badala yake walishirikishwa wadau wengine wasiojua kero ambao sio wakazi wa Manispaa .

“ CDA ilianzishwa Mwaka 1973 kwa kupigiwa kura na  Mikoa yote ya nchi nzima ambapo Mikoa 18 iliunga mkono  na Mikoa mitatu ilipinga lakini Wananchi hawakushirikishwa, cha kushangaza Mamlaka hii  imekuwa ikijifanyia mambo kiholeala tena kwa uzembe,”Alisema Kanyama.

Mjumbe huyo wa NEC alisema kuwa kufuatia kuwepo kwa suala hilo,tayari Baraza la Madiwani kwa kushirikiana na Wabunge wa Manispaa hiyo imeandaa hoja 78 kwa ajili ya kuwapelekea Mamlaka CDA .

Ili iweze kuwajibu na endapo Mamlaka hiyo itawapa majibu ambayo hayaridhishi watalazimika kwenda kwa Rais ambaye ndio mwamuzi wa mwisho juu ya Ardhi.

Kanyama ambaye pia ni Mwanasheria wa CCM, alisema kuwa anashangazwa na kitendo cha Mamlaka hiyo  kuwafanya wakazi wa Manispaa ya Dodoma kama kaburi kutokana na unyanyasaji wa kuwabomolea Nyumba zao ikiwemo kuwanyang’anya maeneo yao huku ikiwapunja fidia.

Awali Wakazi  wa Kitongoji cha Mji Mwema kupitia Katibu kata wa CCM Chang'ombe Suleiman Mringo wakitioa malalamiko yao mbele ya Mjumbe huyo wa NEC,walisema Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA),imekuwa ikiwafanya  waishi kama Wanyama wa porini  kutokana na kuhofia kubomolewa Nyumba zao kwa madai ya kuambiwa  kuwa ni wavamizi.

“Hivi sasa tunaishi kama digidigi  wakati maeneo yetu haya tayari tuna Miundombinu mbalimbali ikiwemo Shule ya Msingi na Sekondari  na watoto wetu  wanasoma je hii ni haki? tutaenda wapi ,kwa maana hiyo tunaiomba Serikali itusaidie tuweze kupimiwa maeneo yetu,” Walisema.

Mjumbe wa NEC ya CCM Taifa Anthony Kanyama anayecheka katikati akiwa na vingozi wa chama hicho wa kata ya Chang'ombe walipokuwa kwenye maadhimisho ya miaka 37 ya CCM.
Akinamama wakazi wa kitongoji cha Mji mwema manispaa ya Dodoma wakiselebuka wakati walipokuwa wakumsindikia Diwani wao Bakari Fundikila aliyekuwa akijiandaa kuwasilisha ujumbe kwa mgeni rasimi.

No comments:

Post a Comment