Tuesday, February 11, 2014

Maduka yafungwa Dodoma wenyewe wagomea mashine za kieletroniki EFDs za TRA.

Wapita njia wakipita katika mtaa wa barabara ya sita  wakishuhudia
maduka yakiwa yamefungwa kwa muda usiojulikana baada ya
wafanyabiashara kugomea mashine za kieletroniki EFDs zilizotolewa na
Mamraka ya mapato Tanzania [TRA]

Baadhi ya wafanyabiashara wa maduka wakipiga soga nje ya maduka yao
baada ya kuyafunga kwa muda usiyojulikana wakipinga mashine ya
kielektroniki EFDs iliyotolewa na TRA na kutakiwa kila mfanyabiashara
kuwa nayo.

Maduka yakiwa yamefungwa katika mitaa mbalimbali ya manispaa ya Dodoma
baada ya wafanyabiashara kugoma kuazia jana karibu nchi nzima kwa muda
usiyojulikana huku mapendekezo yao kuwa gharama za uendeshaji mashine
hizo zifanywe na serekali.

 PICHA NA JOHN BANDA.

No comments:

Post a Comment