Tuesday, September 2, 2014

WANAWAKE WATISHIA KUTOPIGA KURA YA MAONI KATIKA MCHAKATO WA KATIBA MPYA.

Na John Banda, Dodoma
Wanawake nchini wametishia kutoshiliki katika upigaji kula ya maoni iwapo
mapendekezo yenye madai ya haki za wanawake na watoto hayataingizwa katika
rasmu ya pili ya katiba.

Tishio la wanawake hao walipokutana kwenye bunge  kivuli la katiba
lililofanyika mjini Dodoma likiwakutanisha wanawake toka mashirika
mbalimbali yanayotetea haki za wanawake na watoto.

Mmoja wa wajumbe wa Bunge hilo Neema Komba alisema endapo madai yao ya
msingi hayataingia katika rasmu ya katiba watahamasisha wanawake nchi nzima
ili wasikubali kupiga kula ya maoni ili kuikubali rasmu hiyo.

Mjumbe huyo wa Bunge Kivuli alisema wakati mchakato wa katiba mpya
unaendelea wanataka haki
za ndoa, wanawake na watoto ziingizwe kabla ya upigaji kula za maoni.

Aidha amesema ndani ya katiba kuwekwe kipengele kitakachoainisha namna ya
upatikanaji wa haki zao kutokana na kipindi chote cha miaka 50, kukosa haki
ya umiliki ardhi, na rasilimali nyingine za nchi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa mtandao wa kijinsia Tanzania [TGNP] Anna Sangai
amesema katiba itamke na kubainisha wazi madai ya msingi ya wanawake ambayo
ni kumi na mbili yakiwemo umri wa mtoto kuolewa kuanzia 18 mpaka 21, umiliki
na mengineyo.

Bunge hilo kivuli limekua katika majadiliano kwa siku mbili huku
baadhi ya wajumbe wa bunge maarumu la katiba linaloendelea Dodoma
wakawepo kama wageni wasikilizaji likihudhuliwa na jumala ya wanawake
mia tatu
Mmoja wa wajumbe wa Bunge Kivuli la katiba akifafanua jambo alipokua
akichangia moja ya hoja zilizokuwa zikijadiliwa, zaidi ya wanawake 300
wamekutana na kutoa maoni mbalimbali kuhusu haki za wanawake na watoto
ili yaingizwe kwenye Rasmu ya pili ya katiba kabla ya kurudishwa kwa
wananchi mjini Dodoma
Wanawake toka makundi mbalimbali yakiwemo walemavu wakiwa katika
ukumbi wa mikutano katika hotel ya Royal mjini Dodoma walipokua kwenye
Bunge Kivuli la katiba.


No comments:

Post a Comment