Saturday, September 27, 2014

LULU ZA TANZANIA KATIKA MAENDELEO YA TAIFA LETU.





















Na Kandakuwawi Mganda, Dodoma
KIMYA kingi kina mshindo mkuu: huu ni msemo wa wahenga ambao msemaji
wake alikua na maana ya matokeo makuu kwa kila mwenye kusubili
[subila], hali hiyo humuonyesha mtu huyo kuwa ni muungwana wa maneno
akisubili vitendo.
Kuna misemo mingi yanamna hii yenye maana mbalimbali ambayo huanza
kufundishwa kuanzia Elimu ya msingi ili kuwajengea watoto wa taifa
hili muelekeo wa maisha ndani na nje taifa hili.
Matunda ya mtu aliyeyapokea mafunzo kama hayo vizuri toka kwa walimu,
wazazi au walezi wake huonekana kwenye mijumuiko ya kijamii na hasa
linapokuja swala la kimaendeleo.
Bila shaka mtu kama huyo lazima ajulikane kiutendaji hasa kama amewahi
kuwa katika nafasi yoyote ya kiuongozi iwe ya chini kama mjumbe wa
nyumba kumi, kumi au ya juu kama uwaziri na nyinginezo bila kuwa na
majivuno yoyote.
Na hata linapokuja swala la kuwa anahitaji kitu si mwepesi wa kusema
ni mwepesi wa kutoa maelekezo katika makundi mbalimbali ya kijamii bila
kujali yale ya chini yaani wasiosoma na masikini lakini wasomi na
matajili na hata siku akifungua kinywa hukosoa viongozi au wale
waendao kinyume na maadili ya jamii au hata kisiasa.
Ona mtu mwenye sifa kemkem kama Prof Mark Mwandosya ambaye pamoja na
kuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais [kazi maalu] aliye wahi kushika
nyadhifa nyingine nyingi zikiwemo uwaziri huku akijenga wasifu wake kwa
kugombea nafasi ya urais 2005 akiingia tatu bora na Rais wa sasa Dkt
Jakaya Kikwete na Dkt Salim Ahmed Salim.
Akikaa kimya baada ya jina lake kuondolewa na kikwete kuchukua nafasi
hiyo ya ugombea, bado mpaka sasa Prof Mwandosya anaona kazi hiyo ya
urais siyo kazi rahisi ya kumpa mtu anayejifunza uongozi na hasa wa
kisiasa bali hupewa mtu mwenye uadilifu anayejua kuendeleza
alichokikuta.
Prof Mwandosya  siyo mroho wa kutaka mambo kwa pupa karidhika na
Uwaziri huo unaichagizwa na Ubunge wa jimbo la Rungwe Mashariki [CCM]
ndiyo maana mpaka sasa hana alilolisema kuhusu nafasi ya Rais katika
uchaguzi ujao mwakani amekuwa mtulivu sana tofauti na wengine ambao
wameshacheza rafu kwa kuvunja kanuni za chama chao kwa kutangaza nia zao
mapema.
pengine kutosema kwake lolote mpaka sasa anasubili kuwasuprise
wananchi ngoja tuone Prof subila yavuta heri hata kama hutagombea
nafasi hiyo wengi twatakiwa kujifunza kwako.
Wananchi wakati wanasubili kwa hamu nani watatangaza nia ya kugombea
nafasi hiyo ya uongozi yenye hadhi kubwa ili ibaki nafasi ya kutoa
hukumu ya kura.

No comments:

Post a Comment