Tuesday, March 25, 2014

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI ZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI MKOANI DODOMA.


Waziri Mkuu mizengo pinda akisalimiana na viongozi wa serikali na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoa Dodoma muda mfupi mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya jamhuri mjini Dodoma kuhitimisha maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa mkoani dodoma machi 22.
Teknolojia rahisi ya uvunaji maji ya mvua kwenye majengo/makazi yetu ni moja kati ya elimu iliyowavutia wananchi wengi wakati wote wa maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa mkoani dodoma yaliyoambatana na maonesho ya huduma za maji kwenye viwanja vya jamhuri mjini Dodoma kuanzia machi 16 had 22, 2014.

 Baadhi ya maafisa wa ngazi za juu wa baadhi ya  vyombo vya ulinzi na usalama mkoa Dodoma wakipata ufafanuzi juu ya pampu za kuvuta na kusukuma maji; elimu juu ya vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya maji, uhifadhi na utunzaji vyanzo na rasilimali za maji zilitolewa kwa wingi kwenye maadhimisho hayo yaliyoambatana na maonesho ya huduma za maji kwenye viwanja vya jamhuri mjini Dodoma.              

No comments:

Post a Comment