Monday, March 10, 2014

AL-AHL CHUPUCHUPU WATOKEA KWENYE TUNDU LA SINDANO KWAO-ILA YANGA KIBOKO YAO.


Mchezo wa raundi ya pili wa Klabu Bingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya wenyeji Al Ahly imemalizika usiku huu, huku 
Mabingwa hao wa Afrika wakitokea kwenye tundu la sindano baada ya kupata ushindi wa penati 4-3.

Katika mikwaju ya penati, Mabeki Mbuyu Twite na Oscar Joshua walikosa baada ya penalti zao kupanguliwa.

Kipa Deo Munishi aliswazisha makosa yao baada ya kupangua penalti 2.  Ilikuwa ni zamu ya Said Bahanuzi ambaye kama angefunga, basi Yanga ingefuzu.

Lakini mkwaju aliopiga ulitoka nje na baada ya hapo, Ahly wakamalizia penati moja na kufuzu kwenye hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwa hisani ya Salehjembe

No comments:

Post a Comment