Wednesday, June 11, 2014

TAASISI YA KIISLAM YA WAAHMADIYYA YASAIDIA VISIMA VYA MAJI NCHINI VYENYE THAMANI YA 109 MILION

Na John Banda,Dodoma.
WANANCHI wa vijiji mbalimbali vya Tanzania Bara na Visiwani ambao
hawakuwa na maji kwa muda mrefu wamepata neema ya baada ya
kuchimbiwa, kujengewa na kukarabatiwa visima vya maji vya zaidi ya
shilingi  milioni 109 na taasisi ya kiisilam ya Ahmadiyya Jamaat
inayojishughulisha na huduma za kijamii.

Shekhe wa Mikoa ya kanda ya kati kwa mikoa ya Dodoma na Singida  wa Jumuiya
hiyo
ya Waisilam Waahmadiyya Tanzania Bashart ur Rehman Butt,alisema kuwa
kati ya visima hivyo vilivyochimbwa vipya ni 20 na vilivyokarabatiwa
25.

Alibainisha kuwa visima vipya 20 walichimba na kujenga kwa kiasi cha
milioni 94.5 na visima 25 vilivyofanyiwa ukarabati vilighalimu 15,
milioni ambayo jumla 109.5 mil wakiwa na lengo la kuwasaidia
kuondokana na kero hiyo ya ukosefu wa maji katika vijiji hivyo ambavyo
akina mama walikuwa wanatafuta maji kwa umbali wa km zaidi 6,

alisema pamoja na maji hayo kufuatwa mbali bado walikuwa
wakishirikiana kwa matumizi na mifugo huku wanafunzi wa shule zilizopo
katika vijiji hivyo kulazimika kwenda mashuleni na maji bila kujali
umbali walikokuwa wanatoka.

“Chakusikitisha zaidi vijiji vingi vilivyosaidiwa tumekuta wakazi wake
wanatembea mwendo mrefu kusaka maji safi na salama na hata hivyo maji hayo
yanatuwa na mifugo huku wanafunzi wakilazimishwa kufika na maji
mashuleni”alisema

Aidha Rehman Butt alisema kati ya visima hivyo vilivyokarabatiwa miongoni
mwake vipo vinavyomilikiwa na serikali,na vinavyo simamiwa na jumuiya
ya Ahmadiyya Tanzania.
Shekhe huyo hata hivyo alisema kuwa pamoja na uchimbaji na ukarabati
wa visima pia jumuiya imejiwekea mkakati ya kuwawekea Solor Sisitimu
kwa wananchi wa vijijni ambao hawatarajii kuipata Nishati hiyo ya
umeme kuanzia mwaka mpya wa fedha utakaoanza Julai mwaka huu.

Aidha alisema kwa mikoa ya Dodoma na Singida tayari baadhi ya vijiji
vimekarabatiwa  visima vyao ambavyo vilikuwa vimekufa na kujengewa
vipya.
Alitaja vijijii hivyo ambavyo na idadi yake kwenye mabano ni Ng’ambi
(2) Kitumbili (2) na Kinyeto (1) vyote vya Mkoa wa Singida kwa upande
wa Mkoa wa Dodoma ni  vijiji vya Kigwe (2) Ibiwa (2) ambavyo hata
hivyo vilikuwa vimekufa.

Jumuia hiyo iliyoingia kwa mara ya kwanza nchini mwaka 1935 kwa lengo
la kuisaidia jamii katika maeneo ya Maji, Afya na Elimu kauli mbiu yao
ni Upendo kwa Wote, Chuki si kwa Yeyote.
Mwisho.


Wananchi wa kijiji cha Kitumbili kilichopo Singida wakiangali maji
yanayotoka katika bomba la kisima cha kupampu mara baada ya kukamilika
matengezo yake na kukabidhiwa kwa ajili ya matumizi, ambapo ukarabati
wa kisima hicho kilichokuwa kimejifukia ulifanya na Taasisi ya Kiislam
ya Ahmadiyya Jamat inayojishuhulisha na huduma za kijamii

Mtoto mkazi wa kijiji cha Ibihwa Wilayani Bahi akikinga maji
yanayotoka katika bomba la kisima cha kupampu kwa furaha kutokana na
kukosa maji kwa muda mrefu kutokana na bomba la kisima hicho
kuhalibika kabla ya kutengenezewa tena kwa msaada wa Taasisi ya
Kiislamu ya Ahmadiyya Jamaat
Mtoto mkazi wa kijiji cha Ibihwa Wilayani Bahi akikinga maji
yanayotoka katika bomba la kisima cha kupampu kwa furaha kutokana na
kukosa maji kwa muda mrefu kutokana na bomba la kisima hicho
kuhalibika kabla ya kutengenezewa tena kwa msaada wa Taasisi ya
Kiislamu ya Ahmadiyya Jamaat

No comments:

Post a Comment