Monday, June 2, 2014

RAIS KENYATTA AINGIA UWANJANI NA GARI LILIFUNIKWA KWA VIOO VYA KUZUIA RISASI KUHOFU AL-SHABAB.


Rais wa Kenye Uhuru Kenyatta, aliwashangaza maelfu ya wananchi waliojitokeza katika Uwanja wa Nyayo kushuhudia sherehe za Madaraka Day, baada ya kutinga uwanjani hapo akiwa katika gari jipya lililozungushiwa Vioo maalum vya kuzuia risasi kupenya.

Hii imeelezwa kuwa ni mara ya kwanza kwa rais huyo na marais wpte waliopita, kuingia uwanjani katika sherehe za wazi akiwa katika gari la aina hiyo, tofauti na ilivyozoeleka kuingia uwanjani akiwa katika gari la wazi.

Wengi walielezea jambo hilo kuwa huenda ni kujihami na mashambulio dhidi ya kundi la Al-Shabaab, wanaoendelea kuitesa Kenya kila kukicha kwa mashambulio yasiyotabirika wala kutegemewa.

No comments:

Post a Comment