Sunday, June 29, 2014

BAADHI YA ABIRIA DODOMA WASHINDWA KUSAFIRI KUTOKANA NA UHABA WA USAFIRI BAADA YA BUNGE LA BAJETI KUMALIZIKA NA VYUO KUFUNGA

Na John Banda, Dodoma
DODOMA imekumbwa na uhaba wa usafiri wa mabasi ya kwenda mikoani
kutokana na vyuo vikuu na vile vya kawada kufungwa katika kipindi
kimoja hali iliyowasababishia  abiria usumbufu mkubwa ikiwa ni pamoja
na nauri kupanda kinyemela.
Wanafunzi hao hasa wa Vyuo vikuu vya Dodoma [UDOM],  Mtakatifu Yohana,
Mipango na Maendeleo Vijijini [IRDP] na kile cha Biashara [CBE]
ambavyo vina wanafunzi wengi vimefungwa kwa likizo ya miezi mitatu.
Wakiongea na mwandishi wa habari hizi walipokutwa wamezagaa katika
kituo cha mabasi ya kwenda mikoani walisema leo ni siku ya tatu tangu
kuusotea usafiri huo bila mafanikio.
Neema Binamu alisema kutokana na wanafunzi wa vyuo vyote kukutana kwa
pamoja kusaka usafiri imekuwa shida kutokana na Idadi ndogo ya mabasi.
Hali iliyosababisha wenye magari wasiyowaaminifu kupandisha bei
kinyemela mpaka kufikia 30,000 badala ya 17000 na wanapolipa kiasi
hicho huandikiwa nauri ya kawaida tofauti na hapo hakuna
anaesikilizwa.

‘’Kikubwa ni kwa vyombo vinavyohusika na usafirishaji vinatakiwa
kujipanga mapema hasa wakati wa misimu kama hii ambayo vyuo vinafungwa
ili kutuepushia usumbufu ambao hata hatujui kama tutondoka au la’’,
alisema
Kwa upande wao baadhi ya maajenti ambao hawakutaka kuandikwa majina
yao walisema vipindi kama hivi ni vya neema kwao kutokana na siku za
kawaida kura dagaa na sasa watakura kuku takribani wiki nzima.
Nae Mmoja wa askari wa usalama barabarani aliyekuwepo kituoni hapo
alisema yeye si msemaji lakini swala Nauri ya mabasi imegwanyika
katika Madaraja matatu ambapo ni 23,000 lile la kwanza na 17,000 la
tatu.
Na kuhusu upandishwaji nauri kiholela alisema hilo wanalo na
wanawapitia abiria wanaosubili usafiri na kuwapa elimu ili wasilipe
zaidi ya nauri iliyowekwa halali.
Askari polisi anayelinda usalama wa abiria na mali zao katika
kituo cha mabasi yaendayo mikoani akijalibu kutoa maelekezo kwa
wanafunzi wa UDOM waliofika kutafuta usafiri kituoni hapo na kukuta
hali ya usafiri hailidhishi kutokana na uchache wa Mabasi.
Baadhi ya Abiria wakitafakari na mabegi yao baada ya kufika kituo
cha mabasi ya kwenda mikoani na kujikuta wakikosa usafiri kutokana na
uchache wa mabasi ulisababishwa na vyuo vilivyopo mkoani Dodoma
kufungwa kwa wakati mmoja

No comments:

Post a Comment