
KISUTU:
 Mahakama imemuachia huru mfanyabiashara Yusuf Manji katika kesi ya 
uhujumu uchumi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) kuwasilisha
 hati mahakamani hapo ikionyesha kuwa hana nia ya kuendelea na kesi 
dhidi yake.
Manji
 na watuhumiwa wenzake watatu walikuwa wakikabiliwa na mashtaka saba 
yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa
 Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) 
na wa Commanding Officer Korogwe na plate number mbili za magari ya 
serikali.
Watuhumiwa
 wengine walioachiwa huru kwenye kesi hiyo ni Deogratius Kasinda na 
Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja.

 
No comments:
Post a Comment