Friday, April 14, 2017

MAUAJI YA KUTISHA MKOANI PWANI ,MAJAMBAZI YAUA POLISI 7.OPARATION YA KUWASAKA WAUAJI YAANZA.


picha za baadhi ya askari waliouwawa


Na Mathias Canal, Dar es salaam

Askari wa jeshi la Polisi Mkoani Pwani Jana waliwaua watu wanne watuhumiwa  katika majibizano ya risasi Mara baada ya kutokea Mauaji ya Askari nane waliokuwa wanatoka kubadilishana Rindo katika Barabara ya Dar es salaam- Lindi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo (CP) Nsato Marijani Mssanzya wakati wa mkutano wake na waandishi wa Habari alisema kuwa 
Jana tarehe 13/04/2017 majira ya saa kumi na mbili na robo jioni maeneo ya Mkengeni, Kata ya Mjawa, Wilaya ya Kibiti, Mkoani Pwani, Majambazi ambao idadi yao haijafahamika wakiwa na silaha za Moto walishambulia kwa risasi gari la Polisi lenye namba PT 3713 Toyota Land Cruiser na kuwaua askari hao nane.

Kamishna Mssanzya amewataja askari waliouwawa katika tukio hilo kuwa ni A/INSP Peter Kigugu, F.3451CPL Fransis, F.6990PC Haruna, G.3247 PC Jackson, H.1872 PC Zacharia, H.5503 PC Siwale, H.7629 PC Maswi na H.7680 PC Ayoub.

Kamishna Mssanzya alisema kuwa katika tukio hilo majambazi hayo yalipora silaha saba zikiwemo SMG Nne na Long Range Tatu.

Ameeleza kuwa Mara baada ya tukio hilo hatua za Kiintelijensia na kiupelelezi zilichukuliwa na zilipelekea askari kufuatilia na kubaini maficho ya muda ya majambazi hao na katika majibizano ya risasi majambazi wanne waliuawa na bunduki nne kupatikana, Mbili zikiwa ni zile zilizoibiwa katika tukio la Mkengeni na bunduki mbili zikiwa Mali ya majambazi hayo.

Kamishina Mssanzya amewasihi wananchi wakati Jeshi la Polisi likiendelea kuwatafuta majambazi hao wao kuendelea kuwa watulivu na kuendelee kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi zitakazosaidia ukamataji wa wahalifu hao

No comments:

Post a Comment