Saturday, March 18, 2017

MKUU WA MKOA WA IRINGA ANUSURIKA KIFO GARI LAJERUHI WAWILI WAKIWA KATIKA MAZOEZI .


Askari polisi wakiwa wamemkamata dereva taxi aliyesababisha ajali
mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza kulia akimtazama mmoja kati ya majeruhi waligongwa na gari asubuhi hui wakiwa katika mazoezi
watu wawili wamenusurika kifo baada ya gari dogo aina ya taxi kuwagonga wananchi waliokuwa katika mazoezi asubuhi ya Leo mjini Iringa huku mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza akinusurika

Ajali hiyo imetokea nje ya lango la kamanda wa polisi mkoa dakika tatu baada ya kuanza mazoezi kuelekea uwanja wa samora 

Hata hivyo katika ajali hiyo iliyosababishwa na uzembe wa dereva aliyekaidi amri ya askari wa usalama barabarani ambao walisimamisha gari hilo lililokuwa likitoka mwelekeo mmoja na wafanya mazoezi hao

Majeruhi hao wamepata michubuko kiasi mwilini huku mkuu wa mkoa ambae alikuwa karibu na majeruhi huyo hakuguswa kabisa na gari hilo japo alikuwa karibu na majeruhi hao 

Majeruhi wamekimbizwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa

Habari kamili itakujia hivi punde tunaomba radhi kwa picha zisizo kuwa na ubora

No comments:

Post a Comment