Friday, December 21, 2012

LEMA AIBWAGA CCM MAHAKAMA KUU,SASA NI MBUNGE KAMILI WA ARUSHA MJINI

Habari ziliufikia mtandao huu hivi punde, kutoka Mahakama ya Rufaaa jijini Dar es Salaam, zinasema kuwa, Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema ameshinda rufaa yake ya ubunge na hivyo kurejeshewa nafasi hiyo. Kesi hiyo ya Rufaa ilikuwa inasikilizwa mahakama kuu ya rufaa jijini Dar es salaam, ambapo Lema kwa sasa atakuwa mbunge halali wa Arusha mjini. Lema, alisimamishwa kuitumikia nafasi hiyo ya Ubunge wake kupitia CHADEMA, baada ya kuwapo kwa kesi iliyofunguliwa dhidi yake ya kutoa lugha ya matusi na kejeli kwa mpinzani wake aliyekuwa akigombea nafasi hiyo, kupitia CCM, Batilda Buriani.

No comments:

Post a Comment