Shekh Ponda akisisistiza jambo mbele ya waumini wa Dini ya Kiislamu, wakati akizungumza kwenye Kongamano, jana mjini Morogoro.
Shekh Ponda akisisistiza jambo mbele ya waumini wa Dini ya Kiislamu, wakati akizungumza kwenye Kongamano, jana mjini Morogoro.
Askari wa FFU wakijisogeza kati kati ya uwanja mara baada ya muda wa kongamano kumalizika.
Shekh Ponda, akitambulishwa jukwaani.
Kikosi cha FFU uwanjani.
Shekhe Ponda akiwa amezingirwa na waumini
*******************************************
*SHEKHE PONDA ALIPOTOROSHWA NA MASHEIKH KATIKA JARIBIO YA KUTIWA NGUVUNI NA POLISI MORO.
Na John Nditi, Morogoro.
KATIBU
wa Jumuiya ya Kiislamu nchini , Shekhe Ponda Issa Ponda, jana jioni
alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuumizwa na kitu kinachodhaniwa
kuwa ni risasi kwenye bega lake la kulia wakati akiekelea katika Msikiti
wa Mungu Mmoja Dini Moja wa Mjini Morogoro baada ya kumalizika kwa
kongamano ya Dini ya Kiislamu.
Mkasa
huyo ulitokea majira ya saa 12: 15 za jioni eneo la barabara ya Tumbaku
karibu na Fire, mara baada ya kumaliza kwa Kongamano hilo lililofanyika
kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege, Kata ya Saba Saba ,
Manispaa ya Morogoro.
Shekhe
Ponda alishiriki katika Kongamano hilo lililoandaliwa na Umoja wa
Wahadhiri wa Dini ya Kiislamu Mkoani Morogoro na kufanyika siku ya Idd
Pili kuanza saa nane mchana hadi kumi na mbili jioni ya siku hiyo.
Kongamano
hilo lilipata baraka zote kutoka Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro,
ambalo lilitoa masharti kadhaa ya kuzingatiwa na wazungumzaji ikiwa ni
kutokashifu dini nyingine wala viongozi wa serikali.
Sakata
la kutaka kutiwa mbaroni kwa Shekhe Ponda lilikuja baada ya yeye
kudaiwa kukiuka masharti ya Mahakama aliyopewa baada ya kuhukumiwa
kifungo cha mwaka mmoja nje na kutakiwa kutotenda kosa lolote wakati
akitumikia adhabu hiyo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maadalizi ya Kongamano hilo, Ustaadhi Idd Msema, alidai
kuwa ''Shekhe Ponda baada ya kutoka ndani ya gari eneo la Uwanja wa
Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege, alipofika mita chache katika barabara
ya Tumbaku alitelemka na wakati akitaka kuingia tena garini ilifyuliwa
risasi iliyompiga begani''. alisema Idd
Ustaadh
Msema aliongeza kuwa baada ya kupigwa risasi begani waumini waliokuwa
wameambatana naye walimchukua na kumpakiza kwenye Piki Piki hadi
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ili kupatiwa matibabu.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti huyo, baada ya kufika hospitali, waliona
anacheleweshwa kupatiwa matibabu na ndipo walipoamua kumwondoa na
kumpeka kwenye Hospitali binafsi ambayo hakupenda kuitaja kwa jina.
Akizungumzia
kwa kina hali ya Shekhe Ponda baada ya kujeruhiwa, alisema kuwa yu hai
licha ya kuumia vibaya begani na kwamba wanatarajia kumpekela eneo
jingine hususani Jijini Dar es Salaam kupata matibabu zaidi.
Alisema
viongozi wa Umoja huo hawawezi kuweka wazi sehemu anakotibiwa kwa kuwa
jambo hilo ni la kiusalama zaidi hasa wakati huu ambapo kumekuwa na
sinto fahamu.
Baadhi
ya walinzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro waliozungumza juu
ya tukio hilo , walikiri kuwa Shekhe Ponda alifikshwa hosptalini hapo
kwa usafiri wa Piki piki zikiambatana na nyingine zaidi ya 50 na kuishia
getini.
Walisema
walimwingiza adi mapokezi na kwamba walipoona umati mkubwa upo getini
waliamua kutoa taarifa Polisi kuwa wamevamiwa na watu, ambapo muda si
mrefu Polisi wa FFU waliwasili na gari lao Hospitalini hapo.
Hata
hivyo walinzi hao walisema, baada ya kuona Askari wamefika Hospitalini
hapo, baadhi ya wafuasi wa Shekhe Ponda waliamua kumyanyua na kumbeba
mabegani na kutoka naye mlango mwingine wakimlazimisha mlinzi
kuwafungulia mlango na baadaye wakatokomea naye kwa usafiri wa Pikipiki
kusikojulikana.
Kufikishwa
kwa Sheshe Ponda katika Hospitali ya Rufaa kulithibishwa pia na
Mwenyekiti huyo ambaye alidai kuwa waliamua kumwondoa baada ya kucheewa
kupatiwa huduma.
Baada
ya tukio hilo, uvumi ulisambaa meneo mbalimbali nchini ukidai kuwa
Shekhe Ponda amepigwa risasi na Polisi na kufariki dunia. Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Feustine Shilongine akizungumza na Mwandishi
wa Habari hizi majira ya saa tatu usiku wa Augosti 10, baada ya kutokea
kwa tukio hilo, alisema kuwa hapakuwa na taarifa juu ya kutokea kifo
cha Shekhe Ponda.
“
Nimepingiwa simu zaidi ya 50 , zikiulizia jambo hili...kuwa Ponda
amefariki dunia ...Binafasi nami ninazisikia , ujumbe umesambazwa kwenye
simu za watu mbalimbali...tumezunguka kila mahali hakuna kifo wala
maiti yake ...na vijana wangu wanaendelea kulifuatilia suala hili”
alisema Kamanda huyo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo aliweka wazi kwa kusema kuwa Shekhe Ponda yu hai isipokuwa ameumia vibaya sehemu ya bega .
“
Nipo katika eneo ambalo Shekhe Ponda anapatiwa matibabu...sehemu ambayo
hatuwezi kupataja kiusalama , isipo kuwa ameumia vibaya kwenye bega
lake. Lakini yu hai wala hajafa” alisema Msema. Polisi Mkoani hapa bado
haijatoa taarifa rasmi kuhusiana na sakata hilo, nasi twaendelea
kufuatulia kwa ukaribu.
No comments:
Post a Comment