Raia
wa Bulgaria akiwa chini ya Ulinzi baada ya kupata kichapo kwa kudaiwa
kuiba fedha kwenye mashine ya kutolea fedha (ATM) ya BOA tawi la Mbezi
Beach, jijini Dar es Salaam jana.
***************************************
Msako
wa wezi wa kwenye Mashine za Kutolea Fedha (ATM), umeanza kuzaa matunda
baada ya raia wa Bulgaria kukamatwa akiiba kwenye ATM ya Bank of Africa
(BOA), Tawi la Afrikana, Kinondoni, Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa taarifa za benki, mtuhumiwa huyo ambaye hakutajwa jina lake
alikamatwa baada ya kamera maalumu zilizowekwa kwenye ATM za BOA,
kumtambua kuwa ni mwizi sugu wa benki hiyo anayetafutwa.
Mmoja
wa wafanyakazi wa benki hiyo ambaye hakupenda kutajwa jina kwa kuwa si
msemaji, alisema tukio hilo lilitokea jana saa 12 asubuhi baada ya
mtuhumiwa huyo kuwekewa mitambo maalumu ya kumnasa.
Alisema
benki hiyo ilipelekewa malalamiko na baadhi ya wateja kwamba wakienda
kutoa fedha kwenye ATM wanakuta akaunti zao hazina salio wakati
wanaamini zilikuwa na fedha.
Chanzo
hicho cha habari kilidai kuwa baada ya kupelekewa malalamiko hayo,
waliweka mitambo maalumu ya kuwawezesha walinzi wa maeneo ya ATM za BOA
kumbaini mtu atakayetoa fedha kwa njia ya wizi.
“Kama
Benki tuliweka mtambo maalumu na mtuhumiwa huyo alionekana kwenye
mtambo wetu, hivyo tuliwaagiza walinzi wetu watakapomwona mtu huyo
wamkamate haraka sana,”alisema.
Alisema
mtuhumiwa huyo alianza mchezo huo kwa muda mrefu ambapo kwa kutumia
kadi za ATM zisizojulikana idadi yake, alikuwa anakwenda kwenye ATM
mbalimbali za benki hiyo na kutoa fedha hadi Sh10 milioni.
No comments:
Post a Comment