CHADEMA YATIKISA, NI MABOMU YA MACHOZI KILA KONA YA JIJI LA MWANZA, OFISI, MADUKA YAFUNGWA.
*****************************************************
MAANDAMANO
ya amani yaliyokuwa yameandaliwa na chama cha demokrasia na
maendeleo(chadema) yamegeuka shubiri kwa wakazi wa jiji la Mwanza baada
ya kuibuka mapambano makali baina ya waandamanaji hao na jeshi la polisi
mkoani Mwanza na kusababisha polisi kutumia nguvu kuwatawanya wafuasi
wa chama hicho.
Maandamano
hayo ya amani ambayo yalianzia katika eneo la Buzuruga nje kidogo ya
jiji la Mwanza yalikuwa yakiongozwa na wabunge Highness Kiwia wa
Ilemela pamoja na Ezekiel Wenje kuelekea katika viwanja vya Furahisha
yalilenga kumshinikiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo kutoa barua
zinazodaiwa kuandikwa na ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi kuwarejesha
madiwani watatu waliotimuliwa katika Manispaa ya Ilemela kutokana na
kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo.
Polisi
wenye silaha pamoja na askari kanzu walianza kutanda katika eneo hilo
la Furahisha wakiongozwa na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa
Mwanza RCO Konyo ambaye alikuwa akitumia gari lenye namba za usajili DK
068EXV aina ya Toyota Land Cruiser
Maandamano
hayo ambayo awali yalionekana kana kwamba yangelimalizika salama
yaliwasili katika viwanja vya Furahisha majira ya saa 5.38 huku
yakiongozwa na gari la polisi lenye namba za usajili za nchi ya
Uganda 779 UAG likiwa nimesheheni polisi wenye silaha nzito ikiwa ni
pamoja na mabomu ya machozi na bunduki pamoja na askari kadhaa ambao
walikuwa katikati ya maandamano hayo.
Baada
ya maandamano hayo kuwasili katika viwanja vya Furahisha kwa
amani,waandamaji hao ambao walikuwa na mabango mbalimbali yaliyosomeka
kuwa ‘Matata hatutaki uendelee kuwa Meya wa Ilemela rudia kazi yako ya
awali, na jingine Jaji Sumari tumechoka kuahirisha mara kwa mara kesi
dhidi ya Matata na jingine lililosomeka kuwa RD Ndikilo tunahitaji
barua za kurejeshwa kwa madiwani wetu.
Hata
hivyo tofauti na ilivyokuwa imetangazwa kuwa maandamano hayo ya amani
yangelipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo,hakukuwa na
kiongozi yoyote wa Serikali ambaye alikuwepo uwanjani hapo kupokea
maandamano hayo.
Kufuatia
kutoonekana kwa kiongozi yoyote wa Serikali,viongozi wa chadema pamoja
na wabunge wao walikutana kwa faragha kwa dakika kadhaa kwa ajili ya
kujua hatima ya maandamano hayo ambapo Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje
alipanda jukwaani saa 6.45 na kuwaeleza maelfu ya waandamanaji kuwa
wameamua kumtuma Mbunge wa Ilemela Highnes Kiwia kwenda ofisini kwa Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza kuchukua majibu kwa ajili ya kuwaletea wananchi
walioandamana juu ya hatima ya madiwani hao.
No comments:
Post a Comment