Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha
Mh. Francis Mutungi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wakati wa
hafla fupi ya kuwaapisha majaji 10, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es
Salaam mwaka jana. (Picha na Maktaba).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji
Francis S.K.Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.
Taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam
leo, Jumatatu, Agosti 5, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi,
Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita
Agosti 2, 2013.
Jaji Mutungi anachukua nafasi
iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. John
Tendwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria.
Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
5 Agosti, 2013
No comments:
Post a Comment