Na John Banda, Dodoma
Wafanyabiashara ndago ndogo [Machinga] wamekaidi agizo la Manispaa ya Dodoma la kuwataka wasijenge vibanda katika stendi ya Daladala ya Jamatini mpaka watakapopewa utaratibu.
Machinga hao waliamua kuanza ujenzi mara tu baada ya kamati ya Mipango miji kuondoka katika eneo hilo walipofika kukagua na kufanya uhakiki wa waliokuwepo kabla ya ujenzi wa stendi hiyo kuanza Augost 2012 kama utaratibu ulifuatwa wakati wa ugawaji wa nafasi za kujenga vibanda katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa Machinga hao Haji Kulaya aliwatangazia wanachama wake kuwa waendelee kujenga vibanda vyao ili waweze kuanza biashara zao zilizosimama siku nne zilizopita tangu walipohamishwa toka ilipokuwa standi ya muda ya oil com.
Kulaya alisema wajenge kwa kutumia utaratibu wa walioutumia viongozi kugawa namba zenye majina ya machinga hao huku wakiuka agizo la Mwenyekiti wa kamati ya Mipango Miji Stephen Mwanga aliyewataka kutofanya chochote mpaka watakapopewa maelekezo toka manispaa.
Kamati hiyo ilifika katika stendi hiyo na kutokana na kupokea malalamiko toka miongoni mwa machinga hao ambao hawakuwa wamelidhika kutokana na kuwatuhumu viongozi wao kugawa nafasi kwa upendeleo huku wakiwaingiza watu ambao hawakuwepo awali katika stand hiyo.
Mwenyekiti wa kamati ya mipango miji na mazingira manispaa Stephen Mwanga alikaliliwa kuwa walifika na kuamua kufanya uhakiki kwa wafanyabiashara hao na jumla yao ni 88 tofauti naya viongozi wao waliokuwa na 122 huku wageni hasa wanawake wakipewa kipaumbele.
“Tuliamua kufanya uhakiki ule kwa kutumia watu halisi waliokuwepo kwamaana walijuana kila mtu na jirani yake, tuligundua mama lishe 14, wenye vibanda 69, ugogo na upendo Group 7 jumla 88, huku waliokuwa na mezana,mboga mboga na matunda watafanyiwa utaratibu maarumu ili kuondoa malalamiko”, alisema Mwanga
Aidha aliongeza kuwa wao kama manispaa wenye stend na watu walifika ili kuondoa kelo na malalamiko yaliyokuwepo lakini kama watajenga bila mikataba wajiandae kuondolewa na wasimulaumu mtu nguvu ya Dola itakapotumika.
Kwa upande wake Naibu Meya manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede alisema kutokana na ujenzi wa stendi hiyo kugharim Mabilion ya Fedha wamepanga vibanda vyote vitakavyowekwa katika stend hiyo kuwa na paa moja, Rangi Moja na viwekwe kwenye mcholo.
Ngede aliongeza kuwa watahakikisha kila mtu atakaepata nafasi katika stendi hiyo wataingia nae mkataba na kutokana na orodha waliyo nayo itakuwa rahisi kujua machinga hao wataiingizia Halimashauri pato kiasi gani katika makusanyo.
“Tumejenga Stendi ya Kisasa na kutokana na kuwa huu ni mji wa makao makuu lazima kama inavyo ng’a hivi ndivyo iendelee Kung’aa hata na kwa wenye vibanda ili waendane nayo, na kutokana na mkataba hatutasumbuana na mtu juu ya ukusanyaji wa mapato”, alisema Ngede.
No comments:
Post a Comment