Na
John Banda, Dodoma
MWENYEKITI
wa kamati ya Mipango miji na Mazingira Manisipaa ya Dodoma Stephen Mwanga
Amesimamisha ujenzi wa vibanda vya wafanya Biashara ndogondogo [machinga]
katika stend ya Daladala ya Jamatini baada ya kutolidhishwa na Ugawaji wa
nafasi zao.
Machinga
hao wamesimamishwa kujenga siku ya kwanza tangu stend hiyo kuanza kutumika
baada ya kufungwa mwaka mmoja uliopita ili kupisha ujenzi utakaokidhi haja ya
watumiaji wa magali hayo yanayotoa huduma za usafiri wa ndani ya mji huo.
Mwenyekiti
huyo aliwataka kusimamisha zoezi hilo la ujengaji wa vibanda vya biashara zao
kutokana na kile alichosema ugawaji ugawaji wa nafasi hauzingitia utarabu
kutokana na viongozi wa machinga hao kupewa jukumu la kusimamia.
Mwanga
aliongeza kuwa alifika eneo hilo kutokana na kusikia malalamiko ya baadhi ya
machinga kulalakia kutotendewa haki wakati zoezi la ugawaji likiendelea kwakuwa
wengi wao walijikuta wakiwekwa pembeni tofauti na walipokuwa kabla ujenzi huo
haujaanza Augost 2012.
Alisema
alipofika na kujionea kilichokuwa kikiendelea Stend hapo aliamua kumjulisha
mkurugenzi hali halisi na hivyo kuamuliwa zoezi la ujenzi na uwekaji wa vibanda
lisimamishwe na kamati ndogo iundwe ili ikutane na uongozi wa manispaa ili
walijadili na kuliweka sawa swala hilo.
'
Nimesimamisha ujezi usiendelee kwa sababu mtu akishajenga kumuondoa inakuwa
ngumu, mimi na kamati yangu ya mipango miji na mazingira tutakutana na Meya na
Mkurugenzi wa manispaa ili tulitatue swala hili kwa pamoja na kamati yao mapema
iwezekanavyo ili Abiria waendele kupata mahitaji yao kama kawaida'', alisema
Mwanga
kwa
upande wao baadhi ya Machinga hao walisema viongozi wamejilimbikizia nafasi
zaidi ya moja kwa kutumia majina tofauti mpaka ya wake zao huku sura nyingi
mpya zikipenyezwa hata wakati staend hiyo kabla ya kuhamishwa hawakuwepo huku
nafasi hizo zikibanwa kuwa ndogo na wao kujipendelea nafasi za mwanzo.
Mwenyekiti
wa Wafanyabiashara hao wadogo wadogo Haji kulaya alisema mpangilio huo wa
viongozi hauwezi kubadilishwa kutokana na ramani ya stand hiyo kubadilika kuwa
tofauti na ilivyokuwa mwanzo hali iliyofanya kuwe na mpangilio mpya katika
ugawaji.
ASKARI POLISI WAKISIMAMIA UBOMOAJI WA VIBANDA HIVYObaadhi ya wafanyabiashara wakiokota bidhaa zao zilizomwagika chini wakati wa kukusanya kuondoka kituoni hapo baada ya tangazo la serikali
wengine wakibeba friji kuondoa shemu hiyo ya kituo cha daladala
kama kawaida baada ya tangazo kifuatacho ni utekelezaji hapa tingatinga likiwa kazini kubomoa vibanda vya wafanyabiasha katika eneo hilo la standi mjini dodoma
mbao zikikusanywa baada ya kubomolewa
PICHA NA JOHN BANDA
No comments:
Post a Comment