HABARI ZILIZOUFIKIA
MTANDAO HUU HIVI PUNDE ZINASEMA KUWA WATU WANAODAIWA KUWA MAJAMBAZI WAMEINGIA
KATIKA BENKI YA 'AFRICAN BANK' ILIYOPO MTAA WA LIVING STONE KARIAKOO HUKU
WAKIWA WAMEVALIA MAVAZI YA JESHI LA POLISI, WAKIWA NA SILAHA NA GARI AINA YA
NOAH NA KUCHUKUA PESA KILAINI NA KUONDOKA ZAO.
IMEELEZWA KUWA MAJAMBAZI
HAO WALIPOFIKA NDANI YA BENKI HIYO WALIJITAMBULISHA KUWA WAMEFUATA PESA ZA
KUPELEKA BENKI KUU AMBAPO WALIPEWA MZIGO WOTE HUKU NDANI YAKE KUKIWA NA PESA ZA
KIGENI NA ZA TANZANIA NA KUTOKOMEA KUSIKOJULIKANA.
AIDHA IMEELEZWA KUWA
BAADA YA WATU HAO KUTOKA NJE YA BENKI HIYO WALIINGIA KWENYE GARI HIYO NA
KUONDOKA NA BAADA YA DAKIKA KADHAA WAHUSIKA WALITOKA NJE NA KUANZA KUPIGA KELEE
ZA KUITIWA ''WEZI WEZI JAMANI MAJAMBAZI, WAMETUIBIA''.
LAKINI KELELE HIZO
HAZIKUZA MATUNDA KWANI WATU WALIBAKI WAKIDUWAA KWA JINSI WATU HAO WALIVYOKUWA
WAKIONEKANA KAMA ASKARI WANAOSINDIKIZA MAGARI YENYE PESA NA WAO PIA WAKIJUA NI
KAMA KAWAIDA YA MAGARI YANAYOFIKA KATIKA BENKI HIYO KUCHUKUA PESA KWA AJILI YA
KUPELEKA BENKI KUU.
HABARI HIZI
ZIMEDHIBITISHWA NA KAMANDA WA POLISI WA KANDA MAALUM, SULEIMAN KOVA, ALIYESEMA
KUWA NI KWELI TUKIO HILO LIMETOKEA LEO ASUBUHI MAJIRA YA SAA TATU KASORO NA
KWAMBA ATATOLEA UFAFANUZI KAMILI JUU YA TUKIO HILO BAADA YA KUPATA TAARIFA
KAMILI LEO.
No comments:
Post a Comment