Monday, August 12, 2013

MBUNGE AIKATAA CDA DODOMA.



Na John Banda, Dodoma
Mbunge wa Dodoma Mjini DKT. David Malole ameikataa Mamlaka ya ustawishaji Mkao Makuu [CDA] kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
DKT. Malole aliitoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha iyumbu manisipaa ya Dodoma waliokuwa wamekusanyika mlima wa Bwibwi kupokea wageni waliofika kujionea maajabu ya kisima cha maajabu wakati wa 8/ 8 iliyofanyika kitaifa mkoani humo.
Alisema CDA walipewa jukumu la kuuweka mji katika mpangilio wa makao makuu ya nchi lakini badala ya kufanya hivyo wao wamekuwa wakiwachonganisha wananchi na viongozi wao kutokana na kutumia nguvu na ubabe wa bomoabomoa.
Malole aliweka wazi kuwa kumekuwa na tatizo kubwa la viongozi kutoaminika, kusikilizwa wala kushirikiana katika maendeleo ya kata na vijiji ambavyo Vipo katika mpango wa CDA.
kutokana na wengi wao kuwaza polisi na mabomu vinavyotumika wakati wa kubomoa na kupima mashamba ya wananchi bila kuwambia lolote na wanapohoji huambiwa wakawaulize viongozi wao ambao nao wanakosa majibu ya uhakika.
Mbunge huyo alisema Mamlaka hiyo haihitajiki tena kwani imechangia kuchelewesha maendeleo ikilinganishwa na idadi ya miaka waliyokabidhiwa kuendeleza Mji huo ulio katikati ya nchi
''Hawa jamaa wanagonganisha vichwa vya wananchi na viongozi wao, mimi kama mbunge sitaki kuona wananchi wanateseka eti kwa sababu ya CDA kwani mkoa kama Arusha, Mbeya na Mwanza ilitangazwa kuwa majiji kulikuwa na CDA?'', alihoji Malole

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Iyumbu Yona Ngobito alisema kwa sasa hahitaji kuona CDA alisema kutokana na kulaumiwa na wananchi wake hataki hata kuiona mamlaka hiyo kijijini hapo.
Alisema mwanzoni aliwapokea na kufanya vikao na wananchi kutokana na kutoijua vizuri, kwa sababu mambo yote waliyokubaliana yakiwemo ya fidia na viwanja vya bure kama sehemu ya fidia CDA wameyageka na kuwataka wanchi kulipia Fedha maradufu tofauti na walivyolipwa.
Nae Chifu wa Wagogo Lazaro Chihoma alisema ni afadhari CDA ifutwe kuliko kuachwa ikiwatesa wananchi kwa vitisho vya mabomu toka kwa viongozi wa mamlaka hiyo huku wakiachwa wakiwa masikini wa kutupwa kwa kigezo cha uwekezaji.
Akijibu Tuhuma hizo Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya ustawishaji makao makuu CDA Mtemi John ofisini kwake aliwataka wananchi kuwauliza viongozi wao.
''Sisi tukishajua matumizi ya eneo husika kama mamlaka hatufanyi lolote bila kuwaita vingozi na kuwajulisha hivyo jukumu la kuwajulisha wananchi linabaki mikononi mwao, ndiyo maana tukienda kupima au kubomoa hatuwezi kuzngumza nao'', alisema Mtemi

No comments:

Post a Comment