Moshi.
Mfanyabiashara tajiri wa Mirerani na Jijini Arusha, Erasto Msuya,
ameuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 kwa kutumia bunduki aina ya Sub
Machine Gun (SMG), jana mchana.
Erasto anayemiliki vitega uchumi kadhaa na anayeaminika kuwa miongoni mwa wafanyabiashara wa Mirerani wanaoongoza kwa utajiri,
aliuawa jana saa 7:00 mchana wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
“Eneo
la tukio kumeokotwa maganda karibu 21 ya risasi zinazoaminika ni za
SMG, yaani mwili ni matobo kila sehemu kwa kweli ameuawa kinyama sana,”
alisema polisi mmoja wa Kituo cha Bomang’ombe.
Kufuatia
mauaji hayo yaliyotokea kati ya neo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro (Kia) na mji wa Bomang’ombe, mji huo ulifurika magari ya
wachimbaji kutoka Moshi, Arusha na Mererani.
Habari
za uhakika zilieleza kuwa wauaji wake walikuwa katika pikipiki na baada
ya kumminia risasi hizo, walimpora kibegi ambacho haikujulikana kama
kilikuwa na madini ama mamilioni ya fedha.
Kulingana
na vyanzo vya habari, mfanyabiashara huyo alipigiwa simu na kukubaliana
kukutana katikati ya mji wa Bomang’ombe na makutano ya Barabara ya Kia
katika Barabara Kuu ya Hai kwenda Arusha.
RPC Kilimanjaro afafanua alivyouawa:-
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema kuwa mfanyabiashara
huyo aliuawa saa 7:00 mchana eneo la Mjohoroni kati ya mji wa
Bomang’ombe na makutano ya barabara ya Kia.
“Uchunguzi
wa awali unaonyesha kuwa Eransto alikuwa akitokea Moshi kuelekea
Arusha, na alipofika hilo eneo la Mjohoroni alichepuka na kwenda meta
300 nje ya barabara,” alisema.
Kamanda
Boaz alisema alipofika eneo hilo, alikutana na vijana wawili waliokuwa
na pikipiki ambao waliingia ndani ya gari kwa lengo la kufanya
mazungumzo yanayodhaniwa ni ya kibiashara.
Hata
hivyo, muda mfupi tu Erasto alishuka kwenye gari lake na kuanza
kukimbia na ndipo mmoja kati ya wale vijana alishuka kwenye gari la
Erasto na kuanza kumminia risasi nyingi.
No comments:
Post a Comment