MAKAHABA nchini sasa wanataka watambuliwe na wapewe ulinzi
wanapokuwa kazini, ili na wao watoe kodi kwa serikali.
Kupitia chama chao, Africa Sex Workers’ Alliance (Aswa)
wanawake hao wanasema kwamba biashara yao ni sekta ambayo inatoa fursa nzuri
kwa nchi kujiendeleza kiuchumi.
“Tunataka
watu watuangalie kama tunaoweza kusaidia kukuza uchumi huu na wala si kuangalia
kwamba tunaendeleza mmomonyoko wa maadili. Biashara hii inaajiri mamia, kama si
maelfu ya watu kote barani, akasema mkurugenzi wa chama hicho, Bi Doughtie
Ogutu.
Alisema
chama cha Aswa kilianzishwa mwa madhumuni ya kutetea maslahi ya wanachama ambao
wamepitia mengi, yakiwemo kupigwa, kuuawa na hata kulazimishwa kushiriki ngono
na wanyama miongoni mwa mengine.
Ingawa
wanaamua kuendelea na biashara hiyo, makahaba wanakiri kwamba biashara hiyo ni
hatari, hasa iwapo watapatana na wateja wabaya au hata katika hospitali
wanazokwenda kutibiwa.
Bi
Ogutu anakumbuka miaka minane iliyopita pale mmoja wao alipopata mteja Mzungu
lakini akarejea akiwa maiti. Tena mwanzoni mwa mwaka huu, wasichana wakakamatwa
katika eneo la Pwani wakiwa na mwanamume mwengine wa kigeni na kushtakiwa kwa
kujihusisha na ngono isiyostahili - na mbwa.
“Hao
wasichana hawakufanya hivyo eti kwa sababu walikuwa wakipenda. Walilazimishwa.
Nilienda Mombasa kufuatilia kesi hiyo. Ni kwa sababu wanawake hawa hawalindwi
na sheria. Wateja wao huwadanganya kuwa watawalipa, lakini wanapofika nao
kwenye nyumba zao ambapo hakuna hata anayesikia ukipiga kelele, unafanya nini?”
akauliza.
Kwa
sasa, chama cha Aswa kinapanuka kutoka kuwepo katika mataifa kumi na kinaelekea
Magharibi na Afrika ya Kati. Lakini ushawishi wake hapa Kenya umekumbwa na
changamoto nyingi.
Maandamano
Mwaka
jana mwezi Machi, tawi lake la Kenya Sex Workers Alliance (Keswa) liliandaa
maandamano kwenye barabara za jiji la Nairobi kutaka wafanyakazi hao
watambuliwe, ili wawe wakitozwa ushuru. Keswa walidai kuwa na wanachama 40,000
ambao wanaweza kuchangia pakubwa katika uchumi wa nchi hii.
Lakini
kamati maalum ya Baraza la Jiji wakati huo, iliyoundwa na Meya Goerge Aladwa
kuangalia kama kuna faida ya kuruhusu makahaba kuendeleza biashara yao,
ilikataa mapendekezo ya wanawake hao.
No comments:
Post a Comment